Wakuu hivi ukinunua gari kutoka Zanzibar ukifika Dar ushuru inakuwaje?au ndio wanapiga kama imetokea dubai?wanaofahamu hii kitu hebu watujuze.
Mie sio mtaalam sana wa mambo ya Kodi hizi.Ila nauzofu tu katika kusafirisha gari zangu nikinunua.
Mara nyingi hii inategemea na ushuru uliolipia.
Kuna ushuru tofauti kati ya Freezone ya Zanzibar na Dar.
Sasa ukiipeleka gari Dar utalipia ile Difference TRA.
Mfano Suzuki Carry hapa kwetu hadi iingie njiani kw amie hununua kwa bei isiozidi 5.4m kwenye Yard.
Lakini nilipoisafirisha Dar ilifikia hadi 7m with points.
Kuna siku jamaa alikuja kununuaCoaster huku akaona kapata bei rahisi alivyofika Bandarini akakuta Kodi kubwa kichwa kilimuuma,akaisusia hapo hapo.
Ufupi inategemea ni gari gani umenunua na gharama halisi ulizonunulia na kodi uliolipa wakati inaingia Zanzibar then ukiipeleka Dar unalipia Difference,kwa ufupi kodi za Dar ni kubwa na Zanzibar zipo Chini sana.
Maana hapa Zanzibar ukiwa mnjanja wa Yard hizi unaendesha Carry kwa 5.m na point tena saffii mpya kwa hapa used kwa Duabi,lakini Dar inakubidi ukienda Yard za Dar kwa gari hiyohiyo sio chini ya 7 - 9m.
Kwa ufupi ni kwamba inategemea Aina ya Gari,ukitaja gari gani naweza kukuulizia kwa jamaa mmoja,ila mara nyingi hawa Agents nao wanatofautiana bei kwa senti kidogo.
Watalaam wa michanganua zaidi watakuja