Mugabe wa Bongo
Senior Member
- Apr 14, 2012
- 145
- 72
Magari gani funguka
Mie sio mtaalam sana wa mambo ya Kodi hizi.Ila nauzofu tu katika kusafirisha gari zangu nikinunua.Wakuu hivi ukinunua gari kutoka Zanzibar ukifika Dar ushuru inakuwaje?au ndio wanapiga kama imetokea dubai?wanaofahamu hii kitu hebu watujuze.
Mie sio mtaalam sana wa mambo ya Kodi hizi.Ila nauzofu tu katika kusafirisha gari zangu nikinunua.
Mara nyingi hii inategemea na ushuru uliolipia.
Kuna ushuru tofauti kati ya Freezone ya Zanzibar na Dar.
Sasa ukiipeleka gari Dar utalipia ile Difference TRA.
Mfano Suzuki Carry hapa kwetu hadi iingie njiani kw amie hununua kwa bei isiozidi 5.4m kwenye Yard.
Lakini nilipoisafirisha Dar ilifikia hadi 7m with points.
Kuna siku jamaa alikuja kununuaCoaster huku akaona kapata bei rahisi alivyofika Bandarini akakuta Kodi kubwa kichwa kilimuuma,akaisusia hapo hapo.
Ufupi inategemea ni gari gani umenunua na gharama halisi ulizonunulia na kodi uliolipa wakati inaingia Zanzibar then ukiipeleka Dar unalipia Difference,kwa ufupi kodi za Dar ni kubwa na Zanzibar zipo Chini sana.
Maana hapa Zanzibar ukiwa mnjanja wa Yard hizi unaendesha Carry kwa 5.m na point tena saffii mpya kwa hapa used kwa Duabi,lakini Dar inakubidi ukienda Yard za Dar kwa gari hiyohiyo sio chini ya 7 - 9m.
Kwa ufupi ni kwamba inategemea Aina ya Gari,ukitaja gari gani naweza kukuulizia kwa jamaa mmoja,ila mara nyingi hawa Agents nao wanatofautiana bei kwa senti kidogo.
Watalaam wa michanganua zaidi watakuja
Weka Budget range,
Zipo za kwenye Yard na zipo za mikononi.
mkuu kwa mfano hiyo carry nikiinunua zanzabar kwa 5.4m na nikaisajiri hukohuko kwa nambari za ZnZ (lakini matumizi ya gari yawe bara) je ninapoileta huku bara inakuaje? Nailipia kodi tena ama? (Sijui wanasema hii ni nchi moja!!) hebu naomba nijuze.
Kama alivyokueleza mdau hapo juu,kwamba suala la number za usajili ni mamlaka tofauti za nchi tofauti.mkuu kwa mfano hiyo carry nikiinunua zanzabar kwa 5.4m na nikaisajiri hukohuko kwa nambari za ZnZ (lakini matumizi ya gari yawe bara) je ninapoileta huku bara inakuaje? Nailipia kodi tena ama? (Sijui wanasema hii ni nchi moja!!) hebu naomba nijuze.
Mkuu nataka kujua kote za kwenye Yard na pia hata kwa mtu..binafsi...
Gari kama lexus Rx 2004 new model ni 24 milioni to 26 tena mkononi na sio yard. Ukisafirisha dar ushuru wake might be 5milion to 9 , Em not sure.
Kama unataka urahisi zaidi kwanini usiagize nje? Can cost you about £5700 including shipping. Ushuru zanzibar 5milion to 6 Inategemea agency.
Unaweza save about 6milion
Like this one
Una specifications za gari hizo?maana nikikuulizia kwa mtu kuna maswali kama hayo yatafuata.
Maana matoleo ya gari hizo yapo mengi.
Hembu nipe specifications zake kesho nikuulizie