Kwanza, Kenya huhitaji kibali. Kama ni kibali basi ingelikuwa ni VISA au resident permit.
Unachopaswa kupata wewe ni hati ya kusafiria (passport). Kwa kuwa ni ya ghafla basi inakubidi upate hati ya muda mfupi (temporary). Mathalani huwa ni miezi mitatu.
Fika katika ofisi ya Uhamiaji katika eneo lako ukiwa na taarifa zako sahihi na picha ndogo ya passport ya hivi karibuni na Tsh 20,000 (sijui kama imebadilika ama la). Watakuhoji, kisha wakiridhika watakupatia control number kwa ajili ya kulipia.
Baada ya hapo, watakugongea muhuri na utaendelea na harakati zako. Kumbuka, utapaswa kuchanja chanjo ya homa ya manjano kabla ya kuruhusiwa kuvuka mpaka. Utaenda hospital ya karibu haswa za Wilaya na Mkoa, utachoma chanjo husika na kukukabidhi cheti.
Kila la kheri.