Nataka kufanya biashara ya maua haya ya bandia, una nini cha kunishauri?

Sasa mkuu biashara ya maua na hujui nini maana ya vases unachezea watu akili humu eeh..jana umesema misuli inakuuma..mwehu wewe
😂😂😂sasa kuumwa na biashara wap na wap
matibabu yanahitaj hela we jamaa ebu fungua akili
 
samahani kaka😀😀😀nisamehe kwa kutoelewa mapema
 
maua ya plastic aende kariakooo bhana kule mtaa wa El shadai maduka ya wachina yapo tele wanauza hayo maua na veses zake kwa bei rafiki

kule kuna maua hadi ya 3k ambayo decors wa sinza wanauza 10k -15k
kikubwa ye afanye reseach kwanza

namanga ya sasa si kama ya zamani atakutana na wapigaji wampige asiamini 😂😂😂

naongea nikiwa namanga
 
Miaka ya nyuma nyumba zilipambwa kwa dizaini ya haya maua, kwa sasa sijajua. Ngoja wajuvi waje, kila la kheri.
Siku hizi ni nadra sana kukuta maua au picha ya kuchora ndani ya nyumba, Bongo muvi ni ushahidi tosha, unadhifu wa sebule zetu umetoweka.
 
Kariakoo sio sehemu ya kuulizia watumiaji, ni sehemu ya kuulizia bei na upatikanaji. Hata Namanga wananunua Kariakoo. Namanga ndio watumiaji na ndio wanajua maua gani kwa wakati gani yanauzika. Wapambaji kibao na wakodishaji wa vifaa vya decors wako pale na wanajua trends za soko. So akienda Kariakoo anaulizia maua yapi na ya nini.

Ni sawa mtu anataka kununua Kirikuu au pikipiki la guta unamwambia aende kuulizia showroom wanakouza badala umuelekeze aulize vijiweni wanaonunua hivyo vitu response yao na wanavyotumia.
 
lakini uoni kama muuzaji ndo anajua exactly kipi kinatoka sana kwa wakati fulani kipi hakitoki na wafanya boashara wengi masha’allah sio wachoyo wanakuambia lakini pia aingie mwenyewe kudig in asisubirie kuambiwa afanye upembuzi yakinifu based on eneo analotaka kuweka hiyo biashara yake

maana ukute tunaongea habari ya namanga na kariakoo kumbe mtu yuko nanjilinji
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…