Nataka kufuga ndege tausi

Nataka kufuga ndege tausi

GAMBLER

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2009
Posts
303
Reaction score
11
Salamu
Wapi hapa dar naweza kupata tausi kwa ajili ya kufuga, nauliza pia ni kuwa inaruhusiwa kufuga tausi? Na bei ya tausi mmoja ni sh ngapi??
 
Nijuavyo mm Tausi ni nyaraka za Serikali kwa Tanzania hivyo hairuhusiwi mtu kufuga hao ndege. Na ndio maana ukimgonga unashtakiwa
 
Nimewahi kuwaona ikulu tu so far...sijui kama watu wanafuga!!

Nimewaona hata nje ya kibaha (misugusugu) ni wengi, wanaruka ruka, nadhani hupenda sehemu za kimya sana, hawapendi bughdha. Hata Arusha kuna lodge moja (siikumbuki jina) nimewahi kuwaona, kwa kweli wanapendeza sana, zaidi wanapofunguwa manyoya yao ya mkiani, amazing.
 
Hata chui anaruhusiwa kufugwa mkuu, alimradi ufuate sheria zote za maliasili!
Wasiliana na mamlaka husika kaka.
 
Natamani kufuga ndege aitwae tausi. Sijajua kama raia wa kawaida naweza kufuga ndege hawa maana naona wapo state house na maeneo ya karimjee. Naomba nifahamishwe kama hili linawezekana na wapi naweza kupata vifaranga vya tausi.
 
Fuatilia Maliasili na Utalii ni moja ya viumbe ambavyo Kama utapenda kufuga unatakiwa ukaombe kibali lakini ungekuwa mwarabu labda ungefanya Kama Twiga
 
sijui kama utaweza...but ukiweza tufahamishe aisee..
na mimi nataka kufuga tausi....

from story nilizosikia tausi huwa hawakai kwenye nyumba za 'malofa'
wanakimbia....lol
 
Muulize kikwete wale tausi wa enzi za mwinyi wa ko wapi utajua kama wanafugwa ama wanapelekwa na ndege nje ya nchi
 
Muulize kikwete wale tausi wa enzi za mwinyi wa ko wapi utajua kama wanafugwa ama wanapelekwa na ndege nje ya nchi
Kweli tausi walikuwa wengi sana wakati wa nyerere,mwinyi na mkapa.wamesepa wapi au kuna jini mla tausi magogoni?
 
mkuu kawaone wale wanaoshughuia makaburi Kisutu,ukiwakatia kitu kidogo watakupati mayai yao,lakini hupatikana kwa shida sana.
 
sijui kama utaweza...but ukiweza tufahamishe aisee..
na mimi nataka kufuga tausi....

from story nilizosikia tausi huwa hawakai kwenye nyumba za 'malofa'
wanakimbia....lol

dah! haya fugeni tuje tupige chabo kwenu.
 
Heshima na utii mbele kwenu wakuu,,,,, kuna mabishano yalikuwepo kati yetu ya kuwa eti ndege aina ya tausi huwa hawana kabisa ile kujamiiana kwenye uzao wao, ndipo kwa kujua jamii forum ndio mwisho wa ubishi nikaona nilete hili suala mbele yenu kwa ufafanuzi zaidi. Kwenu waungwana
 
Umemaliza shule za Kata nini? Sasa wamepatikanaje? Kama mmekosa mambo ya kuandika si usome ya wenzako afu ukalale tu.
 
nimekuja mbiombio nikajua labda unao unawauza maana nawatafuta sana hao ndege!

Tukirudi kwenye maada' ulikuwa unabishana na mtu wa namna gani na mlikuwa wapi? maana unaweza kuta mlikuwa mnakunywa ulanzi au mbege ndo mnabishana. maana hayo majibu mliopeana daa! nisawasawa nakusema paka hawapandani kisa haujawahi kuwaona wakifanya hivyo.
 
aise kama ulikuwa una bishana nini sasa wangezalianaje sasa huo ubishi wao hamkuweza hata ku think critically
 
Wapo viumbe hai (wanyama) walioumbwa kipekee na hawajamiiani kama njia ya kudumisha uzao. Wanyama (viumbe) wa namna hiyo hawakuumbwa jike na dume bali wameumbwa wa aina moja mwenye mbegu za kike na kiume. Sivyo walivyo tausi. Hawa wameumbwa dume na jike. Tausi dume kwa kiingereza anaitwa "Peacock" na tausi jike kiingereza anaitwa "Peafowl".

Tausi dume mara nyingi ndiye aliyekivutio kikubwa kwa wanadamu hasa kwa uwezo wake wa kutandaza manyoya yake ya mkia ambayo ni marefu na yana michoro ya rangi nzuri mno, nichoro ambayo binadamu wameiiga mara nyingi katika mavazi hasa ya akima dada/mama. Tausi huyu dume hutandaza manyoya yake kwa sababu kabla ya kupandana lazima tausi "wachezo ngoma", au kwa maneno mengi wanafanya vitendo ambavyo vimeitwa na wanadamu "Peacock mating dance", na shughuli hii hasa hufanywa na tausi dume kuwavutia/kuwaita majike ili wapandane. Tukio hili la dume kuwaita majike ili awapande kwa hakika ni kivutio kikubwa mno kwa wanadamu na kwa kweli uzuri na umuhimu wa kufuga tausi uko katika umbo analoonekana nalo tausi dume wakati huo. Hata lile umbo la tausi wakiwa katika tendo la kupandana ni kivutio kikubwa kwa watazamaji. Fuata link hiyo hapo chini uone tausi wakipandana.

Peacocks mating - YouTube
 
Back
Top Bottom