Kyawanjubu
JF-Expert Member
- May 13, 2017
- 2,452
- 2,197
Kama ukiweza unganisha honeymoon moja kwa moja ukitoka church..Hii imekaaje wazee mwezi December nataka kufunga ndoa KKKT Mbezi dar.Sasa watu wananishangaa kwanini sichangishi na wala siwaambii.Mchungaji wangu ameniambia kazi yake ni kufungisha ndoa hayo ni ziada,
Hii imekaaje? Au mimi ndio wa kwanza kufanya hivi?
Sheria ya wapi hiyoKisheria ndoa lazima iwe na sherehe.Ingawa sheria ya ndoa haijasema sherehe iwe vipi.Kwa hiyo fanyeni sherehe hata ya watu kumi tu haina tatizo.
Unavyopenda sasa sherehe.... Nasubiri kukuona hiyo siku ukicheza kwaitoDadaaaaaa
Kisheria ndoa lazima iwe na sherehe.Ingawa sheria ya ndoa haijasema sherehe iwe vipi.Kwa hiyo fanyeni sherehe hata ya watu kumi tu haina tatizo.
Naona madharau kabisa, tena zinadumu kuliko za sherehe kwenye boat na kumbi mbalimbali.
Ila ya kwangu lazima niwachezeshe kwaito kama navozicheza mimi now
Pourquoi pas??Haaaa haaaa o là là, Ma Cheri ce ne pas bonne 'idée!!
Ahsante sana kwa mawazo na ushauri mzuriWana, JF, ndoa ni mume na mke kuwa pamoja sherehe ni mbwembwe uchwara.
Pana, Bibi zetu zamani wanasema walikuwa wanatoroshwa (nimeisikia hili neno kutoroshwa sana kanda ya ziwa) na ndoa zao zilidumu, na zikawa na furaha na amani.
Mleta Uzi, wewe funga ndoa cha muhimu ishi kwa amani, upendo na furaha na mkeo. Utaona baraka sana maishani mwenu.
Pia, nimetoa "likes kwa comments almost zote" kuonesha kuwa NDOA siyo sherehe Bali ni makubliano ya mtu mume na mtu mke kukubaliana kuishi pamoja kama mke na mume.
Mimi siyo shekhe, Mchungaji au padri, ila viongozi wote hao hawasemi habari za sherehe bali wanasema (mume na mke ndiyo ndoa).
Kila la Heri kwa wote wanaotaka kuwa na wenzi wa maisha (mtu mwanamume na mtu mwanamke) kwa ndoa ya aina hii ya bila sherehe.
Japo, anayependa sherehe na jamii yake inataka kufanya sherehe poa tu ila sherehe isiwe kikwazo cha vijana (wa kiume na kike) kuoana.
[HASHTAG]#emmyta[/HASHTAG]