Wana, JF, ndoa ni mume na mke kuwa pamoja sherehe ni mbwembwe uchwara.
Pana, Bibi zetu zamani wanasema walikuwa wanatoroshwa (nimeisikia hili neno kutoroshwa sana kanda ya ziwa) na ndoa zao zilidumu, na zikawa na furaha na amani.
Mleta Uzi, wewe funga ndoa cha muhimu ishi kwa amani, upendo na furaha na mkeo. Utaona baraka sana maishani mwenu.
Pia, nimetoa "likes kwa comments almost zote" kuonesha kuwa NDOA siyo sherehe Bali ni makubliano ya mtu mume na mtu mke kukubaliana kuishi pamoja kama mke na mume.
Mimi siyo shekhe, Mchungaji au padri, ila viongozi wote hao hawasemi habari za sherehe bali wanasema (mume na mke ndiyo ndoa).
Kila la Heri kwa wote wanaotaka kuwa na wenzi wa maisha (mtu mwanamume na mtu mwanamke) kwa ndoa ya aina hii ya bila sherehe.
Japo, anayependa sherehe na jamii yake inataka kufanya sherehe poa tu ila sherehe isiwe kikwazo cha vijana (wa kiume na kike) kuoana.
[HASHTAG]#emmyta[/HASHTAG]