Nataka kufunga ndoa bila sherehe

Nakuunga mkono100% kazi yakukusanya michango si mchezo kipindi hiki
 
ni kweli mkuu aisee tuache kukariri
 
Safanya linalowezekana hali ni tete!
 
Hata ktk uislam hakuna sheria ya ndoa ni sherehe hakunaaa
Ni wahusika,mashahidi na mawalii wa ndoa tu (baba au kaka wa kutoa tamko?
 
Tena kiislam hizi ndoa za kichamungu
 
Usichangishe, fanya harusi kwako ila angalia mimi yalinikuta haya:
Nilifunga ndoa sitaji wapi ila sikuchangisha, nilimwambia kila mgeni aje na chupa yake ya wine. Nilikuwa na vyakula, vinywaji sisemi mengi maana majanga yalitokea ila ndo hivyo ndoa ilifungwa na sherehe ilifanyika. Wavamizi hawakosi hata ufanyeje tena wabaya kuliko ungealika. Wengi Mungu kawahukumu lakini kwa ubaya waliotufanyia walitanguia ila wazazi wetu wa pande zote walipata chakula ila kilichobaki kiliibiwa na wasaidizi waliojifanya marafiki pamoja na vinywaji vyote.
 
Mimi mwenyewe sikuwahi kuchangisha mtu, ila waliona aibu wengine wakaleta mwenyewe.

Na kwakua ilikuwa sio ya mchango nilifanyia nyumbani kawaida sana, na watu wakala na kunywa.

NOTE:

- Kwasababu hakukuwa na michango sikupata malalamiko ya aina yeyote zaidi ya sifa.
- Watu wote sasa hawanipi kadi as wanajua SITAKAA NICHANGIE KAMWE HARUSI.
 
Hiyo ni poa lakini km unajiweza Fanya sherehe ili iwe ni kama kumbukumbu yako kimaisha.lakini pia inabidi MKE wako aweameridhia usije ukawa umemkwaza maana wanawake wengi wanaamini ndoa bila sherehe ni kama wameporwa
 
Nawafahamu wengi wamefanya hivyo. Unakwenda kanisani baada ya ibada unakuwa umeandaa sehemu ya kupata dinner watu wachache mnafurahi na maisha yanasonga mbele kama waliofunga ndoa zenye sherehe za mamilioni kwa siku moja.
 
Ujinga huo, we put money on long term investments...Mwambie apambane na hali yake, ufahari huo sionagi maana yake!
Namwonea huruma mnoo he's my blood brotha

.....kingine ni mtu peace mnoo, akiwa na hela ujue shida zako zimeisha kwa mda!
 
Uko sawa, sherehe ni mbwembwe tu hazina kizuizi ktk kufunga ndoa. Tena ndoa ikiisha unamwambia na mkeo tangulia nyumbani mimi naenda kuangalia mpira.
Nimeipenda sana hiyo.
 
Kumbe wenye mawazo ya aina yako tupo wengi,ubarikiwe na azma yako mkuu
 
Kisheria ndoa lazima iwe na sherehe.Ingawa sheria ya ndoa haijasema sherehe iwe vipi.Kwa hiyo fanyeni sherehe hata ya watu kumi tu haina tatizo.
Sheria ipi, itaje ni kifungu gani cha sheria.Tuanzie hapo. Ndoa ndiyo ipo kisheria siyo sherehe.
 
Kwa sisi wa msikitini kawaida sana,kwanza sisi ndoa ni sehmu ya ibada,kwa hiyo poa tu,lisongeshe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…