Nataka kufunga ndoa bila sherehe

Nataka kufunga ndoa bila sherehe

Baada ya miaka 6 nahitaji kufunga ndoa na wanawake 4 tofauti tofauti lakini nilikuwa napendekeza kupata roll Royce phantom 2 na sherehe ifanyike kwenye meli kubwa ya kifahari vipi ni vibaya kwani....??
 
Mkuu tuko pamoja.... Hiyo ni namna nzuri sana

Fanya hivi... Alika ndugu jamaa na marafiki wote hapo kanisani, baada ya ibada mnapata kama robo saa ya kuabudu na kusifu kwa shangwe kuu ndani ya kanisa

Baada ya hapo mnapiga picha za ukumbusho nje ya jengo la kanisa kisha kila mtu atawanyike kwenda kwao. Itakua poa sana mkuu usijali

Ntakucheki PM
 
Hii imekaaje wazee mwezi December nataka kufunga ndoa KKKT Mbezi Dar. Sasa watu wananishangaa kwanini sichangishi na wala siwaambii.

Mchungaji wangu ameniambia kazi yake ni kufungisha ndoa hayo ni ziada,
Hii imekaaje? Au mimi ndio wa kwanza kufanya hivi?
Wewe ni wa pili kufanya hivyo,wa kwanza ni Dr.W.P.Slaa
 
Mi sichangiagi na sihudhurii so I guess when time comes it will be my only option
 
Kisheria ndoa lazima iwe na sherehe.Ingawa sheria ya ndoa haijasema sherehe iwe vipi.Kwa hiyo fanyeni sherehe hata ya watu kumi tu haina tatizo.
Samahani mkuu unamaanisha sheria ya nchi gani hapa? Au labda sheria ya ukoo wenu?
 
Mm pia nafunga kimyakimya. Nafunga alfajiri napitiliza ofsin

Sio mbaya, ila ukiifanya mchana kweupe ndio vizuri ili uishinde nafsi yako, JITOE KIFUNGONI. Hakuna anayekudai! kwanini ufunge ndoa usiku usiku!

Wapo watu wengi wana hela ila wanafunga harusi simpo sanaaa.

TUFIKIRI TOFAUTI, TUACHE MAZOEA!
kufunga harusi ya gharama wakati hauna nyumba, Kiwanja au ada ya mtoto ina maana gani? Kama sio ujinga!
 
Safi sana!!!!!! Mabinti ndio wana complicate mambo: ......
Usawa mgumu mazes, so mnaona hata baba toka kando ya ziwa Victoria anavyobana matumizi
 
Mi sichangiagi na sihudhurii so I guess when time comes it will be my only option

We ndo kama mimi kwa kweli sinaga hela ya kuchangia, ni bora nikanunue lori la mchanga nijenge. Na ya kwangu itakapokuja ntafanya staili hii hii
 
Ni wewe tu mnaenda na mashahidi wenu tarehe husika iliyopangwa Safi Kabisa.
Rafiki yangu alioa mchana wa swaum,Akachukua mkewe safari,jioni baada ya iftar upande wa kikeni ukakodi mziki limradi tu washeherekee,kipindi hiko mume na mke wako mbali na eneo husika,Huwa tukiwa na best tuna joke,tulioa mchana wa ramadhani na bado watu waliwasha kigodoro,je ingekuwa siku ya kawaida ? Ktk sherehe za ndoa mengi yasiyompendeza Allah hutokea na ukizingatia ile ni ibada hakuna namna isipokuwa kutafuta jinsi ya kuziepuka.
 
Hii imekaaje wazee mwezi December nataka kufunga ndoa KKKT Mbezi Dar. Sasa watu wananishangaa kwanini sichangishi na wala siwaambii.

Mchungaji wangu ameniambia kazi yake ni kufungisha ndoa hayo ni ziada,
Hii imekaaje? Au mimi ndio wa kwanza kufanya hivi?
Funga ndoa yako kwa salama wewe siyo wa kwanza.Tena utakuwa na amani hizo sherehe ni ziada tu ndugu yangu.
 
Asanteni sana kwa michango yenu, jamiiforums ni zaidi ya mitandao. Hapa ni sehemu sahihi sana
Tulifunga ndoa walikuwepo mashahidi pande zote mbili na kiongozi wa dini.mpaka leo tuna zaidi ya miaka 10.
Kila mtu alikabidhiwa cheti cha ndoa maisha mengine yakaendelea.
 
Ni.fresh tu mkuu japo ukitutangazia humu hata jwa buku 5 tano sio kesi mkuu hata kreti za balimi na azam cola tunapata
 
Back
Top Bottom