Biashara hii ipo vizuri, kwanza kabisa usiogope swala la kwamba kuna maji mengi. Ni kweli maji yapo mengi lakini ukiangalia data bado watanzania wengi wanakunywa maji ya kuchemsha, mbili maji mengi faida ni 60% sababu maji is free commodity. Cha kwanza kabisa kabla ya kujua utatoa wapi maji, weka business plan yako chini kisha tafuta mtu mwenye uwezo wa kusoma na kuelewa business plan muombe aitoe makosa, afanyie smell test kuona kama ina pass.
Kwenye proposal yako jambo kubwa sana ni sales literature na distribution plan. Ukiweza kutuliza kichwa na kutoa product yenye good quality na competitive price na ukatengeneza sales plan ya ukweli, nakupa less than 5 years lazima utakuwa na at least 5-10% market share kwa Tanzania. Kikubwa hapa ni jinsi utakavyo fanya branding ili uwe tofauti na wengine wote. Mfano, nimewaza kipindi fulani kutengeneza high end bottle water kama parrier au Voss ambapo lazima designing ya chupa iwe juu sana na quality ya maji yawe na PH ya world standard. Lakini hii lazima uwe na pesa ya kutosha kufanya advertisement sababu ya watu unao walenga. Au unaweza tengeneza maji ya nyumbani 20 liter, ukawa una supply majumbani na kugawa water dispenser free kwa mtu anasign mkataba wa kupata maji kutoka kwako for 2 years na ordering at least once a month. Believe me dispenser haina gharama yoyote compare na revenue guarantee.
Tuje kwenye production yenyewe, kwanza inategemea vyanzo vya maji. Kama unataka kufanya reverse osmosis haijalishi maji unayatoa wapi. Vifaa vya kuanzia kuchonga chupa (mold) mpaka equipment za kuchuja maji, kujaza kemikali na kuyaweka kwenye chupa jumla yake ni USD 50,000. Hiyo ni china. Kama upo interest zaidi ni inbox nitakupa direct contacts za watu wanaouza. Na kama unataka niangalie proposal yako ukisha andika nicheki pia.