Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Basi leta mchele iwe main business rejareja. 1M nunua nafaka nyingine. 1M lipa kodi, mzani na set up ila kodi isizidi 100k kwa mwezi.Nina mchele tani 2 na 2 m cash mkuu
Asante mkuuBasi leta mchele iwe main business rejareja. 1M nunua nafaka nyingine. 1M lipa kodi, mzani na set up ila kodi isizidi 100k kwa mwezi.
Serikali achana nayo kwanza
Fuata huuu ushauru📌Tani mbili sio mzigo wa kufungua kitu kinaitwa "store ya mchele" tena hapo unataka uutoe Katavi. Hiyo ni kianzio cha kufungua duka la mchele, sio store kibongobongo.
Ukisema store kwa lugha ya mtaani ni kwamba unauza jumla, sasa jumla gani ya tani mbili. Direct cost za mchele huwa ziko juu sana. Faida ya mchele huwa haizidi 200TSH kwa kilo hapo ni maximum, ukipata 50TSH/kg kawaida ukipata 100TSH/kg uko vizuri.
Chukua wastani wa 100TSH/kg zidisha na tani 2 hapo faida ya wastani baada ya kila kitu ni 200,000.
Hiyo ni profit baada ya kutoa ushuru wa kusafirisha, gharama za kusafirisha, kupakia na kushusha, kupaka mafuta, kuuchekecha kwenye mashine (grading), kulipia viroba na packaging, kusafirisha kutoka ambapo gari litaushusha mpaka store yako (probably utaungana na wenzio wanaoshusha soko la Tandika).
Anyway nisiandike sana. Hiyo ni biashara kichaa kwa mpango ulionao na uwezo wako. Najua watakuja motivation speakers wa JF waseme nina wivu na negativity ila nasisitiza kwa kubold na kupigia mstari. Hiyo ni biashara kichaa.
Badala yake bora uanzishe duka (sio store) la nafaka mbalimbali za rejareja. Naona una mtaji mdogo mkuu