Pre GE2025 Nataka kugombea Ubunge mwaka huu

Pre GE2025 Nataka kugombea Ubunge mwaka huu

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Sawa mkuu. Kila juhudi inayofanywa na mtu yoyote huwa lazima iwe na maslahi ila maslahi hayo yatategemea yanaenda wapi??
Yaani unautaka ubunge huku kuandika vizuri tu shida.

Sio 'mtu yoyote' bali 'mtu yeyote'.

Samahani mkuu, kumbe sifa ya mtu kuwa mbunge ni kujia kusoma na kuandika pekee haijalishi umeishia darasa la ngapi.

Kila la heri mkuu.
 
Awali ya yote nawasalimu katika jina la Mungu Baba wa Mbinguni na amani ya Bwana wangu iwe pamoja nanyi.

Mimi kama kijana wa miaka 35 mwenye shahada ya kwanza ya Uchumi na ni mtumishi wa Umma nimeamua kuingia kwenye siasa na nitagombea ubunge mwaka huu kwaani sababu za kugombea ninazo na uwezo wa kupambana ninao ila kwenu wazoevu naomba mawazo yenu kulingana na sababu zangu za kugombea.

1. Kuteta mapinduzi ya kiuchumi jimboni kwa kutafuta wawekezaji kwenye sekta za kilimo cha umwagiliaji ikiwa ni pamoja na kujenga viwanda vya kusindika mazao shamba .

2. Kusogeza huduma za kijamii zenye ubora hasa afya maji na elimu.

3. Kuimarisha huduma za mawasiliano hasa barabara na simu kwaani jimbo tarajiwa Kuna vijiji havina uhakika wa mawasiliano ya simu na hakuna juhudi inayofanywa na Mbunge wetu na mbaya zaidi misitu inateketea kwa kupasua mbao ila hakuna shukrani inayorudi kwa jamii inayolinda misitu hiyo miaka yote na kwa lugha rahisi Jimbo halina mtu sahihi wa kutetea maslahi ya jamii.

4. Kuuongeza udhubutu au kubadili mtazamo kwa vijana ambao wanaamini siasa ni kwa wazee na sio vijana ikiwa ni pamoja na kuogopa kurogwa.

Ninayo mengi kichwani ila nadhani hayo ndiyo ya msingi hasa kuimarisha huduma mhimu za kijamii katika Jimbo lenye Kila kitu ila huduma ni mbaya kwa sababu hakuna mtu sahihi wa kuzisemea.
Naombeni mawazo na ushauri kutoka kwenu ili nijue naingia kwa GIA gani hasa kwenye CHAMA.
4.Kuongeza uthubutu kwa vijana, wanaoogopwa kurogwa na wazee.
Hii ndo point kubwa kwako.
 
Back
Top Bottom