Kwame Nkrumah
JF-Expert Member
- Dec 2, 2008
- 886
- 376
Lazima uwe mbea kama yule anayesema TZ nzima hajaona mahali palipojengwa vizuri kama University of Dodoma! Na pia alisema akiingia madarakani ataleta 'mapinduzi ya kilimo'!
lazima uwe na slogan moja kali sana, kama vile "uwazi na ukweli", " kasi mpya, nguvu mpya na ari mpya",wewe yako iwe KIBOKO CHA MAFISADI, au UFISADI KWANGU MWIKO, au kali zaidi uahidi kufanya kazi bila mshahara.Chakula si nasikia bure ikulu? Hapo utashinda mara moja.
Na lazima upromise ajira milioni tano na maisha bora kwa kila mwanachuo maana wamegoma sana mwaka huu! Lazima uwe mbea tosha..
Uchawi ni lazima pia, tena ukiweza kushambuliwa kwenye kampeni huko Mwanza na kuanguka chini Jangwani, jua ushindi wako utakuwa wa kishindo above 80%....ok?
Exaud,
Kwa nini unataka kwenda ikulu? Nini kinakuvutia (motivation)?
Kwa nini Tanzania Bara na si Tanzania?(au ulimi/vidole vimeteleza🙂?). Kama ni Tanzania Bara nadhani katiba tuliyonayo kwa sasa haitoi hiyo nafasi.
Kama ni Tanzania kwa ujumla, basi ni wazo zuri lakini naona umechelewa kuanza. Kugombea Urais,kwa maoni yangu, unahitaji maandalizi ya si chini ya miaka mitano! 2010 ni 'kesho' tu!. Kutokana na muda, ili umshinde JK, utahitaji nzuvu za ziada. Pamoja na mabo mengine;
-Ni lazima ufahamike vizuri kwa watanzania (hili linahitaji muda na rasilimali)
-Ni lazima uifahamu vizuri Tanzania na watanzania (SWOT analysis inaweza kukusaidia!).
Umesha-recruit campaign manager?
Unataka kugombea urais wa Tanzania Bara?
Weka sawa hapa Mkuu.
SMU,
Unashauri nisubiri mpaka 2015?
Watu wameshauri masuala ya uchawi,kujifunza kudanganya,kutoa ahadi kibao, nk.Wewe hayo unaona ni sawa?
2015 nadhani ni realistic zaidi kuliko 2010. Watanzania wanataka mabadiliko, lakini kwa sehemu kubwa chama dola kimekuwa kikiviza hamu hii ya watanzania.
Siamini uchawi. Kuna njia nyingi za uhakika za kujenga kujiamini (confidence) na kuaminiwa (credibility)zaidi ya waganga wa kienyeji.
Sio lazima kudanganya katika siasa. Unatakiwa kuwa visionary. Ahadi ni lazima zitokane na uelewa wa mambo na uwajibikaji. Ni lazima uwe tayari kusupport ahadi zako kwa kuandaa mikakati madhubuti na yenye kuaminika.
Kama unataka kugombea urais 2015, basi ingekuwa vema kama ungegombea ubunge 2010. Kwani wewe ni mwanachama wa chama gani?
............................................................................................
Lazima pia uwe na fedha nyingi. Kama unafahamiana na Gavana wa Benki Kuu,hiyo itasaidia.
PUNDAMILIA,,
Kimsingi na kivitendo, huyo rais mnayemwita wa Tanzania, ni rais wa Tanzania bara.
Kinadharia, hapo hapaelezeki.Nisije nikazua mjadala kama Zanzibar ni nchi au laa.
Basi niseme Rais wa Tanzania ili iwe rahisi kama mazoea yalivyo.
Lazima uwe fisadi na umezungukwa na marafiki wa kifisadi fisadi vile.