Nataka kuhamia kwangu chumba kimoja nina mke na mtoto wa mwaka mmoja na miezi 6

Nataka kuhamia kwangu chumba kimoja nina mke na mtoto wa mwaka mmoja na miezi 6

Nmeezeka nyumba yote lakini milango na madirisha naona bajeti yangu bado ndogo sana

Nipo na laki 8 mfukoni mawazo yananiambia nimalizie master bedroom nipige gypsum roof floor na plaster na Choon sink la kukaa then ntafurah solar

Naombeni usharudi wenu kwasabb fundi wa gril kaniambia nitafute laki 9 atanipigia milango ya mbele na nyuma na madirisha yote.

Sasa hapa nawaza usiku kucha nipige madirisha na milango ya nje halafu nisubili pesa nyingne nisihamie sasa hivi au nikarabati chumba kimoja halafu nihamie ili nimalizie nikiwa palepale kwangu.

Choo cha kukaa kwani ni lazma??weka sink la kuchuchumaa la 30 elfu k.koo hicho choo cha kukaa tuu bei yake kile kizudi ji 350000 cha kawaida saaana 150000 au used 100000 mpaka 80000 sasa hiyo hela yote si itaishia hapo?
 
Hongera kwa hatua nzuri

Achana na choo cha kukaa weka floor tiles za public toilet na choo cha kuchuchumaa. Weka grils nyumba yote.

Tafuta wavu weka madirishani na grills za mbele na nyuma.
Milango ya ndani weka mapazia. Mlango wa choo tafuta vipande vya bati naamini kunavilivyobaki. Ukiwa na mbao 2 za 4x2 biashara inaisha.

Hamia, hapa utakuwa na nyumba nzima hata ukiwa na mgeni wa dharura utaweza kumpokea.
Kutokea hapa nenda mwendo wa pole

Ni experience yangu binafsi niliyopitia
Huu ni ushauri bora kabisa.

Umekuwa positive sana Mkuu.
 
Wakuu nilitype error nilikua naamaanisha sink la choo sio sink la kukaa.
 
endelea kulipa kodi uliko, usihamie bila kuweka grills na kuziba na wavu kuzuia mbu,

unawajua culex, aedes na anopheles ?

Kataa Malaria na Dengue

Unajua anaishi wapi? Pengine yupo Njombe ambako hakuna mbu kama sehemu za joto!
 
Hahahahaha...............hizi Tozo tumekubali wenyewe kuwa Makondoo

Imagine Nchi zinazojitambua kupanda tu bei Mkate wanaandamana, sisi huku bei za bidhaa zinapanda hata mara mbili ya gharama za awali tunaona kawaida.

Kwa hiyo wakiandamana bei ya mkate inashuka au inakuwaje?
 
Nmeezeka nyumba yote lakini milango na madirisha naona bajeti yangu bado ndogo sana

Nipo na laki 8 mfukoni mawazo yananiambia nimalizie master bedroom nipige gypsum roof floor na plaster na Choon sink la kukaa then ntafurah solar

Naombeni usharudi wenu kwasabb fundi wa gril kaniambia nitafute laki 9 atanipigia milango ya mbele na nyuma na madirisha yote.

Sasa hapa nawaza usiku kucha nipige madirisha na milango ya nje halafu nisubili pesa nyingne nisihamie sasa hivi au nikarabati chumba kimoja halafu nihamie ili nimalizie nikiwa palepale kwangu.

Nakupongeza, na huo ndo uanaume, lakini angalia isije kuwa gharama za usafiri, miundo mbinu, upatikanaji wa maji ni gharama zaidi kulilo kupanga
 
Huwezi amini hiyo nyumba yako ingekuwa ni mtu wa huku kwetu siku nyingi sana angekuwa ameshahamia huku mtu akishapiga tu bati anajiongeza
 
Kwanza hongera sana mkuu kwa hatua hiyo.
My two cents:
Hakikisha usalama kwanza. Yaani grilles, wavu, milango etc. Kwa mimi, comfort kiasi ni muhimu, hivyo ningeangalia kwanza comfort ya familia yangu. Kama choo cha kukaa ni muhimu kwangu na wife, then weka. Una mtoto mdogo, zingatia usafi. Je floor yako itakuwa ngumu kuhakikisha haina vumbi la kupitiliza litaloweza kumsababishia mtoto ama wewe na wife matatizo ya kiafya yatayowasumbua kwa muda mrefu mbeleni? Zingatia namna ya kudeal na hizo changamoto halafu hamia.
 
Back
Top Bottom