Nataka kuingia Kariakoo kibiashara

Frame nzuri ina-range Kati ya 800k- 1.5M

Mfano lile jengo jipya linalotazamana na msikiti wa Idrisa frame pale 900k
Mkuu mpaji simshauri aanze na fremu ya bei hii.

Zipo fremu za 600k kwa kuwa bado anaanza aanzie hapo, ili azoee kwanza na kuona
Mkuu 10m.

Kama unataka ingia fremu na process zingine kutakuwa na insufficient kwa kiasi Fulani.

Most utalipa miezi 12

Let's say unachukua fremu ya 600k_ 700k

600000×12= 7,200,000

Unabaki 2.8M

Mkuu hiyo pesa unaweza nunua mzigo kwa wachina pale pale.

Ila bado ni pesa ndogo.
 
Nasikitika huo mtaji utaishia kwenye kodi ya fremu. Labda uanze kama machinga aliyechangamka Mkuu, ili ujifunze na kuziepewa figisu za hapo Kkoo na icho ndio nachoweza kushauri kwa sasa.
 
Kama inalipa biashara kwa eneo hilo basi faida ni 5m km kodi tu ni 900k
ni kweli akiwa na mzigo mzuri na connection ya wateja sio mwenzetu miezi kadhaa tuu cha msingi connection hio hujengwa kwa uaminifu wako kwa wateja na mjiuze mzigo mzuri unaokimbia ili akimbize arudi kwako mapema nae atawaambia wenzake watajileta ukifanya hivyo kwa wateja watano kila mteja atakuletea mteja.
 
Mkuu mpaji simshauri aanze na fremu ya bei hii.

Zipo fremu za 600k kwa kuwa bado anaanza aanzie hapo, ili azoee kwanza na kuona biashara inaendaje
Npo bize kidogo hapa sema ntajaribu kuandika kibishi!

Frame za hzo Bei zipo....ila zipo sehemu Gani? Kuna biashara kariakoo ukitaka uifanye yenyewe ndo inakulazimisha ufanyike sehemu Gani🤔 mfano muhusika kasema anataka kudeal na cosmetics, kariakoo ukiskia cosmetics tayar akili yako Moja Kwa moja inajua unaenda kupatia wapi na frames nyingi zipo maeneo gani.....Sasa Kwa maeneo hayo Kuna frame ya 600k?

10M ukiwa mzoefu kariakoo unafanya jambo ila ukiwa mgeni kidogo ni kipengele
 
Karibu, ila kwa mtaji wako bado mdogo
 
Hata mitaa ya amani na kibambawe majengo yapo yanajengwa japo sidhani kama atawahi
 
Kama unaijua kituo Cha POLICE msimbazi, au kituo Cha mwendokasi msimbazi B Kuna njia unaifuata hatua 15-20 unafikia jengo husika
Pia kuna jengo wameanza kubomoa wanajenga jipya karibu na mataa kama unaelekea gerezani huo huo upande wa sandaland ajaribu japo itachukua muda na pia kwa location hio kodi itakuwa juu
 
Hata mitaa ya amani na kibambawe majengo yapo yanajengwa japo sidhani kama atawahi
Watu wanamwaga zege chini lakini anatokea mtu analipia floor ya 4 afanye store yake ya mizigo, ujue saiv uchumi umeachia ndo mda wa kufanya mambo chap chap hatujui 2025 ataingia nani na atakujaje?

Tena saiv hamna task force, TRA hawakabii juu, risiti sio vurugu kama zamani kidogo hamna mizigo kukamatwa
 
Frame kariakoo unalipa mwaka 😁sio kama hzi nyumbani zetu za kupanga tabata barracuda, ila kwenye miamala hata akitengeneza sehemu huo mtaji unatosha
 
Kabisa kama hela basi kwa sasa hela ipo juzi nimepita Kigamboni nimeona nyumba nyingi zinateremshwa na maghorofa kibao
 
DUH MSHAHARA WA NTUUUUU UNENDA UNGUZAAAAAAAAAAA ASEWEEEEEEEEEEEEEEE NGOJA NIENDELEE KUSOMAA COMMENTS
 
Naonaga ni risk kubwa kuanza biashara k/koo.

Ila ukiweza kuishinda hiyo hofu hakyanani we ni tajiri.
 
Anakuja mteha mmoja tuu anafunga mzigo woote akauze mkoani
 
fanya uanze na kigoli ambapo utakuwa unalipia laki mbili au tatu kwa mwezi kusema uanze na fremu kubwa hiyo pesa haitoshi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…