Nataka kuingia kinyang'anyiro cha Ubunge jimbo la Kwela, nipeni data!


jamani wewe sisi tutakukosoaje wakati hatukujui,hatujui sera zako
kwa kifupi hatuna personal profile ya kwako inakuja kweli ?????
 
Mkuu Malinga, usisikie vitisho vya watu kuwa eti jamaa sijui na mchawi au nini. Jimbo la Kwela linahitaji mabadiliko na kwa kuanzia ni kumchomoa huyo jamaa.
Tatizo lako ni kuwa hujatoa details kama kweli ni mwana sisiem kweli na una ushawishi gani katika chama na hasa huku Kwela.
Karibu sana mzee mimi nitakuwa mmoja wa timu ya kampeni endapo utakuwa na sera nzuri kwa maendeleo ya Jimbo letu.
 
Mitanzania ni mioga kweli kweli na imani za uchawi na ushirikina zimewajaa. Ni kutokana na ujinga huo, watu kama akina Mzindakaya wanapeta miaka yote hiyo huenda bila kufanya la maana lolote kule Kwela.

Malinga, nakushauri zingatia mawazo chanya mbalimbali yaliyotolewa hapa. Achana na hao waoga ambao shauri ya uoga wao hakuna wanachoweza kufanikiwa maana kila failure wataiambatanisha na uchawi.

Hakuna mwenye hati miliki kwenye jimbo. Muhimu ni kuwaelemisha wananchi ili wajue uko upande wao; upande wa kutetea hali zao na maslahi yao na sio kwamba unatafuta hiyo kazi kwasababu za kuchuma baada ya kushindwa kupata pesa kupitia kazi zako za sasa.

Tanzania inahitaji mabadiliko na kadri watu wengi wapya na wenye mawazo mapya watakavyoamua kugombea, itakuwa bora kwa nchi yetu.

Nakutakia mafanikio mema. Kumbuka watu wengi watakaogombea 2010 wanaishi mbali na yaliko majimbo wanayogombea. Muhimu ni kuwa karibu na wananchi na wakuelewe dhamira yako.
 
kina mzindakaya wanatishia nyau tu lazima mapinduzi yafanywe
 

Ndugu yangu sina cha kukuelezea privately zaidi ya kurudia kusema kuwa hufai hata kuwa mwenyekiti wa kitongoji.

Kwanza jiunge na unachokipenda, unachoamini kinaweza kukusaidia kutimiza ndoto zako, halafu uanze kujifunza siasa na taratibu za chama chako kabla ya kufikiria kuwa kiongozi.

Binafsi nakuona huna sifa ya kuwa Mwakilishi wa watu zaidi ya kuwa mdadisi tu.
 

Malinga usitishwe na yeyote, wewe zingatia watu wa kwela wanataka nini, na je wako tayari kufanya mabadiliko? kama babu huyo wameshamchoka utachukua na atatoka tu, mfano ni mwaka 1980 au 1985 pale Tingatinga Malechela watu wa Mvumi Dodoma walipomchoka na kumweka injinia kijana aliyekuwa anafanya kazi Mwadui, jina sikumbuki vizuri lakini nafikiri aliitwa Mazengo, huyu bwana alimshikisha adabu mzee yule kwani mambo yake wakati ule hayakuwa tofauti sana na Mzindakaya kwa watu wa jimbo lake, hata hivyo nakutakia mema mbele ya safari hata kama utajikwaa lakini utakuwa umesogea mbele
 

mwanzo kabisa niliona ni kama kamchezo vile, post yako ya pili nikaona upo serious, sasa kama unahitaji msaada kutoak hapa JF hebu fanya haya

1)weka hapa profile yako
2)una cheo au sifa gani ndani ya CCM
3) unafahamika kwa kiwago gani hapo Kwela
4)weka baadhi ya sera zako huku ukitupa sababu za hizo sera (kwamba hiyo sera umeiweka kwa sababu sera ya mzindakaya ilishindwa)
5) mwisho tueleze mchakato wako wa kugombea upo vipi( unaanzia wapi na kuishia wapi)

nadhani hapo unaweZa AT LEAST kupata vitu vya kuanzia
 

Kama unataka kugombea kupitia ccm basi umefulia.Huwezi kupata nafasi ya kushinda kura za maoni kwakuwa wewe ni kijana mdogo kwani ccm hawana sera na vijana.Nyie mtaambiwa subirini ajira milioni 2,hiyo nafasi waachie magwiji ya siasa.Fursa kwa vijana ccm ni finyu mno.........kaa tafakari na uchukue hatua.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…