Ndg zangu wana JF, ninaishi Mwanza, na ni mzaliwa wa mkoa wa Rukwa. Nimesoma thread inayohusu Mrema na Kimaro kule Vunjo; malumbano yao yameibua kitu ndani mwangu, kile nilichokuwa nikikitamani miaka mingi, yaani ukombozi wa jimbo la Kwela. Nimeguswa na kuelewa kwamba siyo tu vunjo inayokaliwa kimabavu na wanasiasa wasio na msaada kwa wananchi, hata Jimbo la Kwela, Sumbawanga (mh Mzindakaya). Nataka nikatoe changamoto na hatimaye kungo'oa kisiki hicho cha mpingo katika kinyang'anyiro cha Ubunge kupitia CCM, kuanzia kura za Maoni.
Sina uzoefu mkuubwa sana katika siasa, lakini elimu yangu ni ya chuo kikuu na uzoefu wa kutosha katika shughuli nyingine za kijamii, siyo siasa.
Ningependa kupata taarifa zifuatazo:
a) Fukuto la uchaguzi la mwakani katika jimbo hilo!
b) Kura za maoni zitafanyika mwezi upi
c) Ni nani na nani ambao wamejitokeza hadi sasa ktk kuonyesha nia ya kuingia katika kinyang'anyiro. Ukimfahamu mshindani wako ni rahisi kumng'oa.
d) Sifa za mtu anayetakiwa kugombea ubunge, kupitia CCM!
Naombeni taarifa za kina zitakazo nisaidia kujipanga vyema.
Nitafurahi kama mtanishirikisha kwa PM (private message) ili msianike mchele kwa kuku wengi.