Nataka kuiona nguvu ya milioni 2 kwenye biashara mpya

Joined
Jul 13, 2019
Posts
51
Reaction score
93
Naweka swala langu hapa nikiamini sijakosea.

Shida yangu kubwa ni namna yakuifanya 2.0Mil ianzishe na kusustain biashara.

Shortly; mimi ni kijana nipo dodoma, nilikua nafanya kazi sehemu flani mkoa jirani, nikapata post ya serikalini, sikuipenda ila wanaonizunguka hasa familia hawakutazama kama nilivyotazama mimi (Najua inafahamika namna gani watu wanatamani kuajiriwa serikalini). Ndoto zangu sio kuajiriwa milele hivyo kwangu haikua golden chance kama walivyoiona wao.

Kiufupi walifanya nikaacha kazi niliyofanya(private) kwaajili ya hiyo post ya serikali ambayo hivi ninavyoandika imeshashindikana (sioni haja yakufafanua hapo)

Kikubwa ni kua baada ya gharama zote zakusatle kwenye kazi mpya iliyoharibika nimejikuta nimebaki na milioni mbili tuu, na sijisikii tena kuomba ajira kwa mtu yeyote maana hata kilicho fanya hiyo kazi mpya kuharibika ni pale mkuu mmoja wa idara alipotaka nimuabudu na kumnyenyekea kupita kiasi ( msiniquote vibaya, mimi niko humble sana tuu, ila kila kitu kina kiasi)

Sasa nataka kufanya biashara simple inayofit kwenye hiyo capital yangu. Nahitaji msaada wa idea inayotekelezeka maana all my life will depend on that.
 
Baadhi ya mawazo niliyonayo.
1- Car wash simple ambayo ntaikuza with time
kuifanya iwe kwenye standard flani.
2- pay point. Mpesa + tigopesa + airtel money n.k. Hii
nayo itaanza na scale ndogo kama mtaji ulivyo,
then ...
3- Darasa la Excel na Computer kwa ujumla. Hili
naona hata kulianza ni issue coz nikijitahidi sana
hiyo hela itanipa computer zakawaida 5 au 6 (nina
uzoefu kidogo pale kariakoo, nawezapata hata 7) so
hela itaisha darasa na vibali ntaangukia pua.

4- Kuuza viatu vya mtumba. Hii sina taarifa zamuhmu,
nikawaza kwenda maimoria (moshi) wale jamaa
huuza viatu bei rahisi sana, so nikifahamu
wanakochukulia patanifaa sana

5- Biashara ya mazao. Hii niliwahi kuifanya 2016
mkoani Njombe, nilifanya kwenye ngano tuu, haiku
mbaya ila nilihitaji kurudi chuo nikamalizie shule.

6- Kununua eneo (shamba), then nifanye ufugaji. Hili
changamoto yake nikwamba ufugaji utanilipa
baada kipindi fulani, sasa huo muda wa katikati
ntaishije?

7- Niende nikasome post graduate diploma ya ualimu
then nikawe mwalimu wa Physics na Mathematics
niwe naandaa lesson plan, D.E.O na R.E.O
wanifokee kama mtoto. Hii nikisoma ni uhakika
maana Physics haina walimu kabisa.

8- .......

Anyway, naomba msaada wa wazo. Hayo yangu saba yasikulimit.

Sijaona umuhimu wakusema elimu yangu hapa ndomana sijaiweka.
 
Iyo namba 7 Si utakua unarudi kule kule usikokutaka mkuu
 
Mkuu piga hiyo Namba 1 muda Wa kupata senti ni mfupi baada tu ya kufungua ... Ukisimama vizuri nakusihi ufungue hiyo biashara Namba 6..
 
Asante mkuu, nimeinote.
Ideas zako ni nzuri ila kuna nyingine mimi naona ni kama kamari. eg kilimo. Ni kizuri lakini unahitaji kuwa stable kimtaji.
1: Car wash: Ukipata sehemu nzuri na uifanye mwenyewe hii ni rahisi kuanza na faida yake inaingia kwa haraka. Cha muhimu ni kupata eneo zuri. Napendekeza uanze na hii.
5. Biashara ya mazao i.e. ngano.: Hii nayo ni nzuri kwa kuwa uliwahi kuifanya, hivyo unajua changamoto na faida zake. Rudia kuifanya na uanze na hiyo ngano, baadae uongeze mazao mengine.
3. Kuuza viatu: Hii ya kuuza viatu vya mtumba nayo ni nzuri kama unajua kulengesha viatu vizuri. Unaweza kuchagua sehemu yenye wanunuzi wengi na wewe ukaweka pale ''goli'' lako. Siri ya hii biashara ni kujua kulengesha vitu vikali. Changanya na nguo za kike kama unaweza kwani wanawake ni wanunuzi wazuri wa nguo. Kwangu mimi hzi ndiyo biashara nimeona zinafaa kuendana na msimamo na mtaji wako
 
Nashukuru mkuu. Ngoja nilione nalo limekaaje japo nilitamani iwe biashara ambayo mimi ni sehemu ya watendaji, sasa kwenye mgahawa najiona nikitakiwa kuajiri na mimi nikiwa muangalizi tuu.
Kama hupo Dodoma fungua mgahawa nina imani kuna population kubwa kwa sasa
 
Asante mkuu, mchango wako umekua wamuhimu sana.
Mpaka sasa naona car wash imekua na credit zaidi. Nikiweza kuifanya mapema ikaniweka stable ntakua nimeuwahi msimu wa ngano kabla haujaisha, then nikafanya kukusanya mzigo kiasi nikauhifadhi.

Asante kwa mara nyingine.
 
Mkuu car wash inalipa na kwa hiyo hela inatosha sana.chukua mashine ya kuoshea magari,bei zake ni 700k-900k japo zipo na kubwa zake.ila kwakuanzia unaweza kuanza na hizo .hapo chukua na tank la lita1000 nazani ni laki3 ,nunua na spray na zaga zaga za urembo wa magari kusha tulia...

Mimi wakati nafukuzia ajira nilifungua car wash kwakweli sikujuta,kwa siku sikuwahi kurud na pesa chini ya 40000 hapo mafuta na maji nishalipia vyote.hiyo ni kibaha tu mzee je dar au dom ....jaribu hiyo mzee
 
Nashukuru mkuu. Ngoja nilione nalo limekaaje japo nilitamani iwe biashara ambayo mimi ni sehemu ya watendaji, sasa kwenye mgahawa najiona nikitakiwa kuajiri na mimi nikiwa muangalizi tuu.
Unaweza ukawa mtendaji pia nakushauri ingia YouTube angalia migahawa inaendeshwaji kwa mtaji mdogo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…