Nataka kuishitaki Faidika Financial Institution

Nataka kuishitaki Faidika Financial Institution

emkey

JF-Expert Member
Joined
Mar 15, 2011
Posts
728
Reaction score
137
habari wanajf.
nlikopa shs 1.2milioni toka faidika july mwaka jana, nikapiga simu kwa wahusika mwezi october wakanisms kuwa nitawalipa shs 3.3milioni kwa miezi 36. zilipotoka salary slip za dec 2014 imeandikwa jumla ni 7,3milioni. naweza kuwashtaki?
 
Ukikwisha washtaki uende ukakope TUNAKOPESHA LTD.
Kifupi hao majamaa ni matapeli.
 
Inategemea ulichukua mkopo wa muda gani. pia usihangaike kuwashtaki wewe subiri wakate deni lao kwa muda wa miezi 10, kisha tafuta pesa kiasi ulichokopa nenda kawaambie unataka kumaliza deni, utajikuta umelipa hiyo hiyo ulichukua. nilifanya hivyo na nilifanikiwa.
 
Sio kila kitu unakimbilia kushitaki. Kushitaki ina maana mna mgogoro ambao mmeshindwa kuutatua nyie pande mbili hivyo mnaiomba mahakama iwasaidie kutatua mgogoro huo. Cha kufanya ni kuwaona wao. Wewe kitakachokulinda ni ule mkataba mlioandikishana...
 
Asanteni kwa ushauri, karatasi za mkataba ninazo, ngoja nifanye hima niwaone.
 
Asanteni kwa ushauri, karatasi za mkataba ninazo, ngoja nifanye hima niwaone.

Hakikisha unatoa copies usitembee kuwaonyedha original copies hafi itakapohitajika kabisa.
 
Back
Top Bottom