Nataka kujaribu Kilimo Cha Samaki

Nataka kujaribu Kilimo Cha Samaki

Job K

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2010
Posts
9,314
Reaction score
7,149
Wakurugenzi habari zenu!

Nimekuwa nikishawishika kujaribu hiki kilimo lakini sijui ABCs za hii shughuli. Kwa ufupi mimi nina shamba langu halo liko Kasulu kando ya mto Ruchugi, shamba hili linakuwa karibu na maji mwaka mzima. Niliweka ndugu zangu pale shambani nikiamini kwamba lingewatoa kimaisha maana mwaka mzima wewe unakuwa na mazao ya kila aina lakini wenyewe wamekuwa wavivu sana! Sasa nimepata wazo la kuanzisha ufugaji wa samaki sijui utanitoa? Naomba wadau wenye uzoefu na hii shughuli wanipe maoni yao na namna bora ya kufanikisha zoezi hili! Je kwa hapa nchini ni wadau gani wanatoa ufadhili wa kilimo cha samaki?
 
Shughuli hiyo ni nzuri na inalipa sana kama utaweka nia na utakuwa tayari kufanya hivyo

Lakin Kwa upande wa wafadhili ngoja waje wenye kuwajua watujuze.
 
ufadhili ni mgumu kwa project kama hiyo, japo wapo; labda mkopo, kama una sifa za kukopesheka..watafute Equity bank...sina hakika na uwepo wao huko kigoma. Ila najua kuna mtu nilimwandikia Bplan ya Fish farming huko Chalinze na akapata mkopo wake..saivi amevuna mara mbili....mafishi kibao!! kama vipi karibu nikuandikie mradi huo
 
Asante kiongozi, bahati mbaya hapo kwenye red na mimi ni mtaalam wa hizo mambo maana nimefaya kozi ya AEA 210 Agribusiness and Entrepreneurship Development, nimepigwa msasa na Dr. Makindara niko vizuri, ha ha ha haaaa Ipilimo ong'wise imekula kwako!!
 
Hivi samaki wanalimwa au wanafugwa? Wataalamu wa Kiswahili tusaidieni.
Ha ha ha haaaa! Dogo hicho Kiswahili kimetoholewa kutoka kwenye Kiingereza (Fish farming), si unajua tena lugha ya malkia mpaka watu wanakimbia vikao unacheza wewe.
 
Hivi samaki wanalimwa au wanafugwa? Wataalamu wa Kiswahili tusaidieni.
Aisee kwa mara ya kwanza ndio nasikia samaki wanalimwa
Ngoja jamaa awalime baada ya kuwapalilia na trekta kisha kuwanyeshea maji kuwavuna kwa combine harvester na kuwasaga akimaliza mimi nitakua mteja wake wa kwanza kununua magunia 10
 
Back
Top Bottom