Nataka kujilipua na CARINA TI nisaidieni bei za yard Bongo

😲😲😲😲😲 hizi ni gari za wapi?

Wakuu,

Baada ya kuhanya sana huku na kule na kuona mipango ya kuweza kujenga mjini kabla ya kununua usafiri inazidi kwenda kombo kwa upande wangu,

Nataka nijilipue tu ninunue gari ya watu wa uwezo wa chini tu,
Ambapo nitaisajili kuwa ya biashara ili niifanye Uber ambayo nitaendesha mwenyewe pindi nimalizapo mizunguko yangu binafsi (lengo ni kupata japo hela ya wese na services ndogondogo, badala ya kuipark tu).

Choice yangu ni CARINA Ti angalau ya mwaka 2001, yenye CC 1490.

Kwa nini CARINA Ti?
Kwa sababu nina lengo la kukaa nalo kwa zaidi ya minne (4) uzima ukiwepo na ikiwa halitapata hitilafu kubwa kwani inaonekana aina hii ni gari ngumu-

Na kwa kuwa uwezo na mpango wa kubadilisha ndani ya muda mfupi haupo,
Hii itanifaa kwani nitajikita sana kwenye kuzingatia zile services za msingi kwa wakati.

Sasa kwa kuwa sina imani sana kuhusu kununua ya mkononi kwa mtu (iliyotumika Bongo),
Naomba kwa wenye kujua mnijuze bei ya hiyo gari tajwa katika yard za Bongo na/au ikiwezekana gharama ya kuagiza (used from Japan) mpaka kuiweka barabarani.

(Kuhusu kupitwa na wakati/kutokuwa la kisasa- hilo nalifahamu, na halinipi shida)

Natanguliza shukrani.
 
Chukua TI mkuu ni gari ambayo ngumu na haishuki bei kama IST mkuu jiandae na milioni 11.5 hadi 12 unapata kisu kabisa ndani kinanukia harufu ile ya japan. Usisahau kwenda kwa dick sound magomeni kufunga mziki mkuu the rest enjoy life and welcome to the world. Alafu wale mademu wote waliokua wanakuzingua saizi utawagonja cha muhimu tembea na kondom kwenye gari mkuu.
Nisaidie juu ya uzembe Gani nikifanya gari inaibwa. Nawazaga Sana jamaa wanaoibiwa magari. Nimepata kesi kadhaa. Huwa wanakosea wapi. Asante
 
Mbwembe na ushamba wa kupenda kuning'iniza funguo kila unapotembea, make sure unapofika mahala na gari yako ipaki endelea na shughuli zako, si kila mtu anatakiwa afahamu kwamba wewe una gari sababu kama una gari ni una gari tu hata watu wasipoona umeshika funguo. Kingine hakikisha unaweka security system ya uhakika sio zile za Lumumba.
 
Wakuu,

Baada ya kuhanya sana huku na kule na kuona mipango ya kuweza kujenga mjini kabla ya kununua usafiri inazidi kwenda kombo kwa upande wangu,

Nataka nijilipue tu ninunue gari ya watu wa uwezo wa chini tu,
Ambapo nitaisajili kuwa ya biashara ili niifanye Uber ambayo nitaendesha mwenyewe pindi nimalizapo mizunguko yangu binafsi (lengo ni kupata japo hela ya wese na services ndogondogo, badala ya kuipark tu).

Choice yangu ni CARINA Ti angalau ya mwaka 2001, yenye CC 1490.

Kwa nini CARINA Ti?
Kwa sababu nina lengo la kukaa nalo kwa zaidi ya minne (4) uzima ukiwepo na ikiwa halitapata hitilafu kubwa kwani inaonekana aina hii ni gari ngumu-

Na kwa kuwa uwezo na mpango wa kubadilisha ndani ya muda mfupi haupo,
Hii itanifaa kwani nitajikita sana kwenye kuzingatia zile services za msingi kwa wakati.

Sasa kwa kuwa sina imani sana kuhusu kununua ya mkononi kwa mtu (iliyotumika Bongo),
Naomba kwa wenye kujua mnijuze bei ya hiyo gari tajwa katika yard za Bongo na/au ikiwezekana gharama ya kuagiza (used from Japan) mpaka kuiweka barabarani.

(Kuhusu kupitwa na wakati/kutokuwa la kisasa- hilo nalifahamu, na halinipi shida)

Natanguliza shukrani.
Carina ni roho ya paka, gari nzuri sana. Naitumia hapa kuja kazini napark mpaka jioni, siku tatu vits na tatu carina.
Kwa Uber kwa nn usinunue Vits au Ractis?
 
Nisaidie juu ya uzembe Gani nikifanya gari inaibwa. Nawazaga Sana jamaa wanaoibiwa magari. Nimepata kesi kadhaa. Huwa wanakosea wapi. Asante
kuwa makini tu na kuilaza sehem salama pia kama unapokaa kuna wizi sana funga GPS uwe una itrack kwenye simu gari ikiibiwa
 
Carina ni roho ya paka, gari nzuri sana. Naitumia hapa kuja kazini napark mpaka jioni, siku tatu vits na tatu carina.
Kwa Uber kwa nn usinunue Vits au Ractis?
Nina miaka 52 naishi jijini DSM sijawahi kuingia barabarani na usafiri je nitaweza. Ninakauwoga flani.

Si unajua mambo ya kuchelewa kutusua!?
 
ingia tu mkuu unakaa nyuma ya lori tu hadi unafika safari yako cha muhim kujiamini mfano mimi nilikua muoga kwenye mataa ile ikiwaka kijani basi nikiwa nyuma ya gari haina shida sema ikawa inatokea mimi ndio niko mbele naamua destiny ya wote walionyuma mwanzo ilikua ngumu badae nikazoea
 
Asante
 
huwezi nunua gari then mvua zikinyesha unawaza nitapita wapi.Ukifanya maamuzi ya magari fanya utakayotumia miaka na miaka kusave some other cost. Gari iwe multi purpose
Gari multi-purpose ipoje?
 
Back
Top Bottom