Kwanza kabisa unatakiwa ujue kuwa ukitaka kujiunga na Jesuit Fathers lazima upitie hatua zifuatazo
1. Unapojiunga nao lazima utasoma philosophy kwa miaka 2-4 kulingana na level yako ya elimu
2. Baada ya kumaliza philosophy utaingia katika utume (regency). Hapa unaingia kushiriki shughuli za kitume katika shirika kwa miaka 2 hadi 3.
3. Baada ya kazi za utume. Unasoma Theology miaka 4. By universal canonical law, kila candidate wa priestly ordination lazima asome Theology kwa miaka minne. Theology ni elimu ya Mungu.
'Theo' means God and 'ology' means study of. So Theology means "Study of God".
4. Baada ya miaka 4 ya Theology kinachofuata katika hatua ya nne ni 'Ordination'. Hapa ndio unakuwa padre sasa. Ukishakuwa ordained unaweza kupewa majukumu ya kitume sehemu mbalimbali linapohudumu shirika au kupelekwa kwenye masomo zaidi.
Baada ya hapo kuna hatua nyingine za mbele zaidi ikiwemo viapo mbalimbali ambavyo vita determine level yako katika shirika.
Hayo nadhani ni baadhi ya mambo machache ya muhimu unayopaswa kuyajua.
I stand to be corrected kwa pale ambapo nimekosea. Hii ni kutokana na experience yangu niliyokuwa nayo.