Nataka kujua ubora wa mbolea ya super grow

Mkuu hii kitu (supergro) sio mbolea. Haijatengenezwa kwa ajili hiyo na wala haina maelezo rasmi ya kutumika kama mbolea.

Sijui ilianzaje hii mpaka wauzaji wao (sio kampuni) wakaanza kuitangaza kama mbolea, lkn hakuna popote Supergro imeshauriwa kutumika kama mbolea au kirutubisho kwa mazao.

Siku za nyuma kidogo (nimeambatanisha ushahidi) uongozi wa NeoLife ulitolea ufafanuzi juu hilo suala na kukiri kuwa sio mbolea na sio sahihi kuiuza kama mbolea.

Kwa bahati nzuri hata wizara ya kilimo (ingawa kwa kuchelewa sana) wametoa katazo rasmi kuhusu Supergro (nimeambatanisha).

Bottom line: supergro sio mbolea, na ni marufuku kuitangaza na kuiuza kama mbolea (Wizara ya Kilimo). Sasa linabaki kuwa suala la imani kwa mtu mmoja mmoja na kwa utashi wake tu!

Ushahidi...
Kanusho la Uongozi wa NeoLife:
View: https://youtu.be/lHMw9FMdTYw?si=lDjAnp8i0VxBThnB
Katazo la Wizara ya Kilimo:

View: https://youtu.be/dOmnwbb4nKc?si=eJ99EXDdA4e2PHCc
Wako,
Mtalula Mohamed,
Mtaalam na mshauri wa masuala ya Kilimo
Mogriculture Tz
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…