Nataka kujua ubora wa mbolea ya super grow

Nataka kujua ubora wa mbolea ya super grow

Heshima yenu wakuu!

Mwenye kujua au aliyewahi kutumia mbolea hii ya maji almaarufu Kwa jina la supergrow. Je nikweli Ipo Vizuri ukilinganisha na mbolea hizi tulizo zoea kama NPK, CAN, UREA, DAP nk?

Nimeifatilia sana Kwa wauzaji wakiinidi kuwa Ina ubora wa Hali ya juu sana kuzidi mbolea zote maji na hata kama hujaweka mbolea ya kupandia basi super grow ndo mwisho wa yote!

Naomba Kwa Ambae anaifahamu Kwa nmna Moja au nyingine hii anipe uzoefu wake hasa yule aliye itumia ilimpa matokeo chanya?

Na pia nitaigunduaje hii ni original na fake? Vipi kuhusu muuonekano huu hapa ipi nzuri kati ya blue na white au ubora sawa ila vifungashio tu ndo tofauti?

Wapi naweza pata original nahitaji naianze na lita5 kama itaonekana inafaa na Ina ubora zaidi. Ahsantee sana.

View attachment 2812765View attachment 2812766
Mkuu hii kitu (supergro) sio mbolea. Haijatengenezwa kwa ajili hiyo na wala haina maelezo rasmi ya kutumika kama mbolea.

Sijui ilianzaje hii mpaka wauzaji wao (sio kampuni) wakaanza kuitangaza kama mbolea, lkn hakuna popote Supergro imeshauriwa kutumika kama mbolea au kirutubisho kwa mazao.

Siku za nyuma kidogo (nimeambatanisha ushahidi) uongozi wa NeoLife ulitolea ufafanuzi juu hilo suala na kukiri kuwa sio mbolea na sio sahihi kuiuza kama mbolea.

Kwa bahati nzuri hata wizara ya kilimo (ingawa kwa kuchelewa sana) wametoa katazo rasmi kuhusu Supergro (nimeambatanisha).

Bottom line: supergro sio mbolea, na ni marufuku kuitangaza na kuiuza kama mbolea (Wizara ya Kilimo). Sasa linabaki kuwa suala la imani kwa mtu mmoja mmoja na kwa utashi wake tu!

Ushahidi...
Kanusho la Uongozi wa NeoLife:
View: https://youtu.be/lHMw9FMdTYw?si=lDjAnp8i0VxBThnB

Katazo la Wizara ya Kilimo:

View: https://youtu.be/dOmnwbb4nKc?si=eJ99EXDdA4e2PHCc

Wako,
Mtalula Mohamed,
Mtaalam na mshauri wa masuala ya Kilimo
Mogriculture Tz
 
Back
Top Bottom