Nataka kukopa Shilingi milioni 5 nianze biashara

Watanzania Sijui Tukoje ?
Tuna Roho Mbayaaa Tunazificha Kwa Kuwa Tuna DNA Ya Unafiki.

Ndio Maana Tutakuwa Masikini Wa Kutupa Milele.
Aliyesema hivi ndio ana roho mbaya 'Biashara Ya Mahitaji Ya Majumbani Ni Za Kizamani Na Hazina Mwendeldzo Na Hazifai Kabisa Kwa Kijana Anaefikiria Kwa Karne Ya 21'................

By the way sio watanzania wote ni masikini wa kutupa.
 
Nitajitahid mkuu ule mda wa jioni kuanzia saa kumi mpaka kufunga saa 4 niwepo pamoja ma weekend
Unajua walio sema "Biashara asubuhi,jioni mahesabu"

wana akili sana? unajua waliangalia vitu vingi?

sikushauri kabisa u kope halafu uajiri mtu

hapo ni sawa na umemkopea huyo unaetaka kumuweka asubuhi mpk hyo saa kumi

swali:

una uhakika atairudisha hiyo 5M???? hiyo hela huku JF ni ndogo sana

ila mtaani na kwenye biashara saivi 5M mlima wake si haba mkuu

Hapo hujatuekea RIBA.

Mi simo
 
Duu, pamoja na riba ntarudisha kama 6.2 mil kwa miaka miwil na nusu,

Nifanyeje sasa mana mshahara naona tu haunitoshi zaid ya kunifanya niwe nasubr sms ya nmb kila mwisho mwez ili nilipe maden
 
Nikweli hata mimi nafanya mobile money....ingawa unaweza kupigwa lakini ni rahisi kujua
 
Poor Mentality a.k. Low thinking capacity
Skuizi watu ni Kukopy biashara tu kuanzisha zao hawataki kabisa
 

Diot kabisa kwani wewe hauwezi enda bank ukakopa yani umemgeuza mwenzio fursa akope yeye aweke kwenye biashara yako, acha umak* na kupenda kitonga kama unaona bzness yako inatoka andika proposal au tengeneza business plan uwezi kosa Capital sio kuja subiri wenzako wakope pesa zao wewe uje ujisogeze
 
Muache tu huyo labda ni wale Wa 'tuma kwa namba hii'
 
Sikushauri kufungua Duka hata kidogo,Duka la mahi taji ya nyumbani huwezi toboa ,kwanza ili upate faida kidogo linatakiwa kuuzwa na mtu mmoja tena mwaminifu

Wewe unatumia mkopo alafu unamwajiri mtu,na ukiwa unaingia Hesabu zikienda kombo jibu ni jepesi tulikuwa tunauza wote ,ndio njia Rahisi ya kukuibia

Kumbuka hata kama ni la familia anatakiwa muuzaji mmoja kwani tumetofautia mahitaji MF: ukiuza wewe jioni unaweza sema ngoja nichukua 5000 nijipongeze kwa chochote kumbe asubuhi kijana naye alitumia 10000 kuhonga/kununu chchote kwa chinga/ alimtumia Mzazi au kajiwekea malengo.wife pengine akaingia ata lisaa labda kijana alienda kununua mzigo akachukua naye 500 ya kusuka au kuongezea hitaji lake,Mtoto akisoma gepu ya kula Shule hata 1000, kumbe kwa siku mshatumi Hela nyingi bado Yale ya lazima ,Usafi ,kodi ,halmashauri usafi,umeme ,vocha n.k

Tafuta biashara ata mbaya mtaji mdogo kipato kikubwa ata kuuza Mkaa au unanunua mashine ya Kutengeneza Mkaa kwa kutumia matakataka kazi ambayo hesabu zinajulikana ua mgahawa n.k

Kuna jamaa ana chaneli yake ya Mgahawa mahali akiwaachia vijana kila siku anapitia Elfu Themanini(80000) haina mjadala na hapo weo wameshajilipa.
Jiongeze mkuu Duka hutoboi kwanza yamekuwa mengi siku hizi kila Mtu kazi ni hiyo
 
Muache tu huyo labda ni wale Wa 'tuma kwa namba hii'

Kaka mawazo yangu ni kuwa
Biashara yoyote inatokana na experience hata kwenye kazi za kuajiri nikitu kinacho angaliwa

Biashara pia ina changamoto nyingi, sio lazima uweke 5M yote katika business moja na ndo maana tunasema au kushauri watu wafanye diversification of capital( yaani usiweke mayai yote katika kapu moja tawanya mayai au mtaji wako)
Mfano biashara ikienda mlama inamaana capital yako ya 5M iko mahala pabaya.


Usifanye biashara kisa Juma anafanya na anapata faida
Haujui nyuma ya pazia anachokifanya, biashara zinamambo mengi ukiacha kitu kama Location kinacho pelekea biashara kufanikiwa, kuna Customer care, know how ya business , experience ya biashara unayotaka fungua unayo, Muda wa usimamizi unao?, Gharama za uendeshaji unazijua yaani Operating Cost usije ukawa umeangalia tu kwa macho ukajiridhisha inabidi ufanye reserch mpk ya gharama na wateja kujua kwa wastani wanakuwepo wangapi katika location yako, biashara nyingine watu wanaloga na kufanya makafala so nakuomba ufanye biashara unayoipenda toka moyoni usifanye kwakua unahitaji kufanya ili mkono uende kinywani au ili usogeze maisha.

Sijajua uko Mkoa gani ila kama unataka biashara inayotoka kwa haraka naweza sema ni biashara ya vitu vya electronic accessories kama Simu ( najua na kufahamu unaelewa watumiaji wa simu ni wengi), lakini pia kuna biashara nimeiona watu wanafanya ni ya Taa za Solar ambazo wanatumia watu wa magengeni mbadala wa vibatali na chemli yaani Taa izo zinachagiwa kwa Jua au Umeme jioni wanakuja kodi kwako kwakuwa hawawezi vuta umeme mpk pembezoni mwa barabara na kwa siku wanalipia elfu 1 tu ambapo wanatumia saa moja mpka saa 5 usiku wanarejesha so unaweza ona ukipata watu 20 umeingiza tsh 20,000 per day na nibiashara ya muda mrefu zaidi ila pia biashara nyingine niya Chakula ( watu wanafanya kazi ili wapate kula na kulala mahala pazuri, biashara ya Money transaction


Ila biashara zote izo zinafanywa na watu so ili uweze kutake over ni lazima uende extra na kuadd value katika biashara yako ndipo utakapo weza toboa usipende copy and paste biashara be Unique

Nihayotu ndugu yangu
 
Kuchukua mkopo wa benki na kuanzisha biashara mpya ni hatari zaidi ya hatari.

Chukua mkopo wa kuendeleza biashara na sio kuanza. Biashara mpya zinachangamoto sana. Yaani mpaka isimame unatakiwa upambane jasho na damu.
Anza na mtaji wako kwanza ili hata ukikwama hakuna matata.
 
Ushamgeuza fursa mwenzio dah!
Na mwamba asipokua makini,,, atakuja kuanzisha uzi mwingne akiwa analia lia apa,,,,afikirie anasaidiwa.. Kaitiwa fursa kumbe yy mwenyew ndo fursa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…