Nataka kukopa Shilingi milioni 5 nianze biashara

Tatizo ni mda wa ziada unakuwa mdgo sana, j3 kazn saa moja asbh mpaka saa kumi jioni ukitoka umechoka, jmos usaf, jpil kuabudu ko mda tunakuwa hatunaa
Yaani bado hujaelewa😂, kuna mtu hapo anakulia mingo amekwambia ana-fursa uweke pesa kwenye kampuni lake.
 
Kipindi gani maduka yalikua machache?
 
Na usichokijua wachaga biashara hizo za maduka ziliwatoa na bado zinawatoa mpk leo mpk wamefungua ma biashara makubwa makubwa.

Na hesabu zao hua ni simple tu ubahiri,consistency na
persistence.

We endelea tu kusubiria hizo biashara zinazo-scale.
Nakubaliana naye aliyesema hivyo, mwenye mawazo ya kimkakati kweli hafanyi biashara ya Duka la mahitaji ya nyumbani...Biashara niile inayo Scale na kukua binafsi hakuna biashara nitakuja ifanya kama hii ya duka.
 
Wabongo wakiwa wanataka hela yako wanakuaga na lugha nzuri sana,mambo yakiharibika huko mbele ya safari ukiulizia pesa yako utaambiwa hio mil 5 utasema nayo ni hela ya kunisumbua.Sasa we fanya unachotaka.

Hapo sasa itabidi ajiridhishe kuhusu uimara wa hiyo biashara na kampuni ili asije akapatwa na asiyoyatarajia, na muhimu kama ataridhika na mwenendo wa hiyo biashara/kampuni basi awe sehemu ya control hasa kwenye finances
 
Nilijua tu utakuja kuwa mkali maana watu kama nyie mnaowaona wenzenu kama fursa mkiambiwa ukweli mnaona kabisa ndege anaruka.
Mkuu sijaweka hapa namba ya simu nichangiwe au sijamwambia mtu aniPM.

Nimempa wazo ambalo ana uwezo wa kulikataa kwa 100%

Sijamshikia mtu bunduki kumlazimisha awekeze kwenye wazo langu.

Na kuwekeza kwenye wazo la mtu siyo kumpa msaada, ni jambo la kawaida kwa mtu makini yeote.

Ndio maana sheria ya makampuni ( LLC ) inataka wanahisa kuanzia wawili.

Sasa unaona kama unataka kunipa msaada, wabongo bana daaaaah !!
 
Kukopa uanzishe biashara halafu umweke mtu,hiyo jioni ukija kukaa hata akiamua Kwa siku awe anachukua elf 5 huwezi jua
Hainaga kuhesabu ile
 
Kampuni yako ni ipi na inafanya nini?
 
Duu, pamoja na riba ntarudisha kama 6.2 mil kwa miaka miwil na nusu,

Nifanyeje sasa mana mshahara naona tu haunitoshi zaid ya kunifanya niwe nasubr sms ya nmb kila mwisho mwez ili nilipe maden
Anzisha uwakal mkuu, tia mpesa, tigopesa,equity,nmb n.k hio sio rahisi kuibiwa mkuu hata kama usimamizi utakuwa hafifu.
 
Kampuni yako ni ipi na inafanya nini?
Swali lako haliwezi kujibiwa kwenye public platform Mkuu.

I'm not that desperate, naijua vizuri nchi hii na watanzania.

Kila mtu anajifanya ana uwezo wa kupush mambo kivyake.

Imagine mtu mpaka anatamani sheria ya makampuni ingekuwa inaruhusu mtu mmoja !!

Juzi tu hapa KijanaHuru katoka kuibiwa wazo lake na HKigwangalla unategemea na mimi niweke hapa that easy !!

Angalia kilichomkuta: https://www.jamiiforums.com/threads...a-bilioni-2-kwa-mtaji-wa-milioni-250.1495596/
 
Tuma p.m basi
 
Juzi nilikutana na mtu kwenye Panton Kigamboni anauza ramani za Nyumba.

Baadhi ya watu kama wewe wakawa wanamwomba wazipige picha.

Yalikwa ni maamuzi kukubali au kukataa.

Siwezi kukutumia chochote mkuu.

Relax
Haina kambaya mkuu.
 
Habari yako.
Kwanza nianze kwa kukupongeza Mwalimu kwa mawazo ya kujikwamua kwenye rat race ambayo yatakupelekea uwe na financially freedom.Unajuwa kuishi kwa kutegemea mshahara tu ni utumwa sana na hakuna aliyefanikiwa na kuishi atakavyo kwa kuangalia chanzo kimoja cha pesa(especially salary)

Nimependa sana akili yako inavyokubali challenge kwa baadhi ya watu kupitia maoni Yao. Wazo lako si baya Kama umelifanyia uchunguzi weka imani,jiamini alafu ingia field uanze kazi/Biashara.
Dunia ya leo Kuna watu wengi sana wana mawazo mazuri ya Biashara ila niwachache wanao ingia Katika ulimwengu wa business,hii maana yake ni nini-Ni kuwa na mawazo mazuri ya Biashara pekee haitoshi inahitaji uwe na boldness (ujasiri) ili uanze Biashara.
Umefanya vizuri kuleta wazo lako hapa ili kulipa challenge lakini Katika Dunia ya leo haupaswi kumwambia kila mtu wazo lako la Biashara ili kuepeka negative mind.

Ngoja nikupe short story kuhusu safari yangu ya Biashara.
Mimi ni kijana nina miaka 27 nilimaliza chuo mwaka 2014.Nakumbuka kipindi bado nipo chuo wakati tumepata boom niliwaza ile pesa nitoa kiasi alafu nianzishe Biashara yoyote ile.Kwa kuwa sikutoka Katika familia ya Biashara hivyo nilikuwa sina uzoefu wa Biashara lakini kitu pekee nilichokuwa nacho ni dream.

One of my friends nilimpa wazo langu kuwa nataka nianzishe Biashara tena Biashara ya kutoa huduma ya saloon ya kiume.Rafiki yangu yule Siwezi kumsahau alianza kunikosoa na kuponda wazo langu la Biashara kuwa si zuri haliwezi ku work katika ulimwengu wa Biashara.
Alinipa sababu nyingi sana kama wanavyokupa wewe baadhi ya wachangiaji hapo juu tena zile sababu ambazo unaona ni muhimu kabisa.
Lakini kwa kuwa nilijiamini Basi nilifungua saloon yangu ya kwanza ya kawaida tu mwaka 2012.

Hadi leo ninapoandaki hapa ni jumla ya saloon 3 za kiume na moja ya kike.
Hakuna Biashara mbaya ndugu kama utakuwa una lenga kutatua changamoto fulani fulani katika jamii unayoishi.Leo yule rafiki zangu ambao walikuwa wanaponda wazo langu ndo wamekuwa wananipongeza kila siku kuhusu mafanikio yangu.

Nataka kusema nini,Uli ufanikiwe katika Biashara inatakiwa kwanza ujiamini.
Fanyia kazi wazo lako naamini utafanikiwa.

Nitakuja kuandika kwanini Biashara nyingi za wafanyakazi hazifanikiwa na kupendeza hatua gani unapaswa kuchukua ili usiwe miongoni mwao.
Asante
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…