Siku moja kuna rafiki yangu wakaribu alifiwa na baba ake mdogo kama ujuavyo watanzania tuliowengi tunatabia yakushirikiana katika shida na raha basi siku ya maziko nilikaa pamoja na vijana wenzangu, tulikuwa tukipeana habari mbalimbali kama ujuavyo watu wa rika zinzofanana wanapokaa pamoja huwa haikosekani mada yakuzungumzwa.
Kabla tulianza kuzungumzia habari za uchaguzi kama ujuavyo mwaka 2020 ni mwaka wa uchaguzi mara baada ya mada hii kumalizika basi mmoja wetu alivutiwa na vile nilivyokuwa natoa Elimu pale, katika mazungumzo yale, baada ya mimi kumaliza kuzungumzia suala la uchaguzi, tukaanza kuzungumzia maisha hapo ndipo Yule kijana akaanza kusimulia habari za maisha yake kwanza alianza kwakusimulia ni jinsi gani alivyokuwa akiwatumia mabinti hali ambayo sitoweza kuieleza humu kwani shetani nae anaweza akachukua nafasi katika mioyo yetu iliyo dhaifu na yenye tamaa yakujaribu kila kitu.
Mtoa ushuhuda alisema kuwa alikuwa na rafiki yake wakaribu ambaye alikuwa akifanya nae biashara moja yeye alikuwa akitokea Singida na mwenzake alikuwa ni wakutokea Dodoma hao walikutana katika mji wa Songea. Lakini ghafla tu aliona mwenzake amenunua gari haikupita miezi mingi akaongeza gari nyingine mbili hapo sasa ndio alimstaajabisha kabisa kwakuwa gari hizo alizinunua zikiwa mpya kabisa tofauti na lile gari la mwanzo ambalo alinunua kwa mtu. Mtoa shuhuda anasema kuwa kwakuwa alikuwa na shauku ya kufika pale alipofika mwenzake hivyo alichukua hatua yakwenda nyumbani kwa rafiki yake Mtoa shuhuda alisema alishangazwa na nyumba iliyojengwa na huyo rafiki yake kwani ilikuwa ni nyumba nzuri yenye kupendeza.
Basi alikaribishwa na rafiki yake nae akakaribia basi baada ya salamu Mtoa shuhuda alimuuliza mwenzanke, ”Rafiki yangu sisi wote tumekuja Songea kutafuta na sote tunafanya biashara moja lakini mwenzangu naona unamafanikio makubwa mno hali ambayo mimi natamani kuwa kama wewe tafadhari naomba nipe siri ya mafanikio yako”.
Baada ya maelezo hayo mtoa shuhuda alisema kuwa rafiki yake alimwambia kuwa ondoa shaka utajiri unapatikana kwa njia rahisi sana wewe zunguka tu utaupata yaani aende kwa waganga na pia alimwelekeza kwa mganga aliyempa utajiri. Mtoa shuhuda anasema kwakuwa alikuwa na kiu yakuwa mtu mbele za watu asubuhi iliyofuata alipanda basi mpaka kule alikoelekezwa, Naam mapema sana aliweza kufika kule alikoelekezwa Mtoa shuhuda anasema huko alimkuta babu wa makamo ambae alikuwa akiishi maisha ya kawaida sana Mtoa shuhuda alikaribishwa na Yule babu ambae ni mganga wa kienyeji. Mtoa shuhuda alimwambia mganga yakuwa anashida yakuwa tajiri mganga akamuuliza kweli kijana unataka kuwa tajiri? kiajana akajibu ndio.
Mganga akauliza tena kijana kweli unataka kuwa tajiri kijana akajibu tena ndio mzee naitaji kuwa tajiri. Maana ninarafiki yangu ambae ninafanya nae biashara moja amekuwa tajiri ghafla nae amesema ameupata kwako hivyo naomba msaada wako mzee, basi mzee akamwambia sawa mjukuu nimekuelewa ondoa shaka hapa utajiri upo mwingi sana tena sana, sasa ndani ya miezi sita nitakupatia dawa ambayo utaenda kuitumia ndani ya miezi hiyo sita endapo kuwa itakufaa naomba uje na pia kama haitokufaa basi naomba pia uje nitakubadilishia.
Kiajana alipewa dawa pamoja na maelezo jinsi ya kwenda kuitumia Mtoa shuhuda alisema aliona vyema aende kwanza kwa wazazi wake kisha arudi Songea kwakuanza kufanya kazi zake za kila siku alifanya hivyo.
Siku ilipofika alianza kuitumia ile dawa aliyopewa na mganga wa kienyeji kadiri alivyoelekezwa Na tazama maajabu ya nguvu za giza zinavyofanya kazi, mara alipoanza kuitumia ile dawa alikuwa anapofanya biashara yake alikuwa anapata mara mbili yaani ukienda kununua kwake unapotoa hela labda elfu kumi basi hutoi elfu kumi unatoa elfu ishirini na kama unanunua bidhaa ya laki moja basi unatoa laki mbili hivyo aliweza kuingiza mamilioni ya pesa ndani ya miezi sita Mtoa shuhuda anasema ndani ya hiyo miezi sita alikuwa amepata takribani shilingi milioni tisa ijapokuwa alikuwa akifaya anasa za kila aina lakini pesa ambayo aliipata kama faida ndani mda huo ni kiasi hicho cha milioni tisa.
Mganga alimwambia kuwa unapokuwa unafanya biashara yako naomba tenga fedha kiasi ambayo siku utakayorejea hapa utaileta. Hivyo milioni tisa ndio ilipatikana kwa muda huo.
Siku yakurejea kwa mganga ilifika basi Mtoa shuhuda hakuongeza wala kupunguza siku alienda kwa babu basi alipofika alimkuta mganga yupo nje anaota jua, mtoa shuhuda alisema kuwa alipokelewa vizuri tena sana kisha akaambiwa twende tukaongee ndani walipofika ndani mganga alimuuliza kijana je dawa imekuwa msaada kwako ? nae akajibu mzee dawa imenisaidia tena sana kabisa, mganga aliuliza kijana alijibu tena ndio mzee dawa imenifaa sana ndio maana nimerudi hapa. Mganga akasema sawa kijana, sasa unahitaji mali zako? kijana akajibu ndio mzee kweli? Kijana akajibu tena ndio nahitaji kuwa na mafanikio katika maisha yangu.
Kijana hapa kuna utajiri mwingi sana utaacha wewe wala haukauki sasa kijana wangu naomba nenda kanawe maji katika beseni lile mzee alimuonesha beseni lilo mbele kidogo ya pale walipokuwa wameketi kijana alifanya hivyo.
Alipomaliza kunawa akamwambia afungue ile dawa aliyopewa awali, kijana alianza kuifungua ile dawa taratibu mtoa shuhuda anasema dawa ilikuwa imefungiwa kwa kitambaa cha sanda hilo aliligundua pale alipokuwa akifungua ile dawa taratibu alianza kuingiwa na hofu mara baada yakuingia ndani ya hofu, baada yakugundua kuwa kile itambaa kilichoviligiwa dawa aliyopewa ilikuwa ni SANDA basi aliendelea kufungua mwishowe alikutana na MKONO WA MTU mganga akamuulize hiko ni nini?
kijana akajibu mkono, basi Mganga akamwambia ukihitaji kuwa na mali zako unahitaji kuwa na mkono wako mjukuu wangu, mganganga akaongeza huo mkono siwezi kuuza wala kukupatia tena iisipokuwa ukihitaji kuwa na maisha mazuri yakupasa uwe na mkono wako mwenyewe. Mtoa shuhuda anasema alijiuliza sana ni kivipi ataweza kuwa na mkono wake? babu akamwambia kwani wewe si una mototo (ndio ninae wakike kijana alidakia) mganganga akamwambia sisi atuchagui watoto, ukitaka kuwa na maisha mazuri kijana inakupasa umtoe mtoto wako, Baba yako, Mama yako, pia na kaka yako mkubwa.
Mtoa shuhuda anasema aliishiwa nguvu nakushindwa cha kuongea baada ya mda Yule mganga akasema endapo kama ukikubali wewe utakuwa tajiri mkubwa lakini kama utakataa utakuwa masikini mkubwa.
Mtoa shuhuda alisema kuwa hakuwa tayari kuyaishi maisha yale tena na alikuwa yupo tayari kuwa masikini wa mwisho lakini sio kuwa na utajiri wa kumwaga damu mpaka anatoa simulizi hii alikuwa tayari ni mtu wakawaida sana na huwezi kuamini kuwa alikuwa mtu tajiri.
Ndugu zangu ifike mahali tulizike na kile tulicho nacho maana kitu cha msingi katika maisha yetu chakwanza ni amani mtu ukiwa na amani katika maisha yko utapata kila kitu lakini ukiwa hauna amani amini kuwa utapoteza kila kitu, subira huvuta heri amini kuwa kama unahitaji maisha mazuri yatafika kwa bidii zako na sio kwa kupita njia za mkato mwisho wako utakuwa kituko na jamii itakucheka.

Upvote
4