Nataka kulisaidia Jeshi la Polisi; Muuaji aliyekimbia DSM anaishi hapa

Mnaweza kuona kama mtoa mada mnafki sijui hayamuhusu,mara mbea ngoja niwape kisa kimoja cha kweli nikiwa mkoa fulani alikuja kijana fulani mtaani kwetu alikua ametuzidi kidogo lakini baada ya kukaa kwa muda ndipo tukapata wasaa kidogo wa kumfahamu na tukaja kufahamu kuwa jamaa alipotoka aliwahi kuua mtu kwa kisa cha kipuuzi puuzi tu na kama alikuja kujificha kule na kuroga hivi,basi siku moja vijana wa mtaani wakiwa wnacheza mpira na mwenyewe akiwepo tabia za utotoni goli la kamba ya katani ndo mwamba wa juu so ikawa utata goli au si goli yule bwana akawa analazimisha ni goli na goli kipa anasema si goli basi bwana yule alipotoa panga hatujui ghafla tu akalizamisha kichwani kwa goli kipa paap ,ubongo nje.....nimejaribu kutoa kisa kirefu kidogo kwa maana ifuatayo mtu aliyemwaga damu isiyo na hatia mkono wa damu huwa unamuandama daima hata huyo wasipomuangalia atafanya unyama tena kikubwa tuheshimu uhai.
 
Polisi wanajisifu kua wana intelijensia kubwa waache wao wenyewe wamtafute mtu huyo. Polisi wetu wamezoea kila tukio hadi wapewe feeds toka kwa raia wema. Ila likija swala la siasa ndio kwanza wanapima hadi hisia za wananchi.
Anachokifanya huyu bwana ni sehema ya intelijensia ya Polisi. Huyu bwana inaonekana kama ni mganga wa kienyeji. Na asikwambie mtu, hao jamaa ni sehemu muhimu sana ya intelijensia ya Polisi.
 
Nenda moja kwa moja kwa RPC-TANGA muone yeye mwenyewe personal mwelezee kwa undani, naimani atachukua hatua stahiki Kisha mtuhumiwa atakamatwa na kupelekwa polisi DSM ili kujibu kesi yake!

NB. Wakati unaondoka Kama tatizo ni nauli mwambie kabisa afande nauli sina I hope utapewa.

Endelea kuwa mzalendo kwa nchi yako
 
- Jiandae kuwa kwenye kaselo kadogo huku unaisaidia polisi. Hapa utaacha kazi zako nyingi kuhangaika na kesi ya mpuuzi mmoja.
Unaweza jikuta na wewe unapata kesi. Baada ya kugundua kwann hukureport kwenye kituo chochote?
- Siku ndugu zake wakijua kuwa wewe umemchomea ndugu yao, jiandae kwa lolote.
Sio kumchoma ni uzalendo
 
Yote hayo yanaweza kutokea lakini je vipi wakifanikiwa kumkamata sababu tu mtoa mada alitoa taarifa sahihi?
 
Hivi humu hakuna hata askari mmoja wa geshi la polisi akachukua hizi information kwa kwenda inbox kwa jamaa akapewa jina na mtaa anaoishi mtuhumiwa na jeshi likaanza uchunguzi kimya kimya maana tayari kuna taarifa za kunyooka zimepatikana kwa jamaa mwingine humuhumu..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…