Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ha ha ha ha....Kwa hela hyo utapata tako la sungura
kwanini usitafute yenye tako la mwanamke?[emoji2960]Habari zenu humu ndani? Niende moja kwa moja kwenye hoja ya msingi. Nimefikia uamuzi wa kununua gari iliyotumika hapa Bongo. Gari ninayoitaka ni yenye sifa zifuatazo:
Aina ya gari: Toyota harrier (Tako la nyani)
Mileage : Isizidi Kms 100,000
Ukubwa wa Engine: 2.4
Rangi yeyote isipokuwa nyekundu
Namba kuanzia D
Iwe katika hali nzuri kwa ujumla.
Bajeti yangu ni kati ya Milioni 14-15.
Karibuni tuyajenge.
Asante kwa kutukaribisha ili tuyajenge...
Kwanza kwa hiyo bajeti yako harrier tako la nyani huwezi kupata...labda ukutane na mtu anataka kuuziwa nyumba kwa mikopo ya Bank au aliyekumbwa na matatizo mengine ya kidunia mf kuuguza.
Pili, ni hatari sana kununua gari bongo lenye mileage chini ya 100000...nyingi wamezichakachua kuwavutia wateja coz watu wameshajua kucheza na akili za watanzania..
Fahamu zetu zimetekwa kwenye namba D na mileage chini ya 100k
Tatu, ukinunua tako la nyani kwa bajeti hiyo, nusu ya muda wako wa wiki nzima utautumia garage kuliko kazini au kwa familia yako.
Bajeti hiyo unaweza kupaya Harrier old model namba B au C yenye hali nzuri sana..
Nadhani nimeyajenga kwa kiasi changu.[emoji41][emoji41][emoji41]
Ahsante sana ninaamini kuwa ukidhi haja ya muhitaji kama nilivyofaidika na ujenzi wakao UBARIKIWE SANA
hahahaa....sio tako la paka......wabongo mna mambo nyie?Kwa hela hyo utapata tako la sungura