Asante kwa kutukaribisha ili tuyajenge...
Kwanza kwa hiyo bajeti yako harrier tako la nyani huwezi kupata...labda ukutane na mtu anataka kuuziwa nyumba kwa mikopo ya Bank au aliyekumbwa na matatizo mengine ya kidunia mf kuuguza.
Pili, ni hatari sana kununua gari bongo lenye mileage chini ya 100000...nyingi wamezichakachua kuwavutia wateja coz watu wameshajua kucheza na akili za watanzania..
Fahamu zetu zimetekwa kwenye namba D na mileage chini ya 100k
Tatu, ukinunua tako la nyani kwa bajeti hiyo, nusu ya muda wako wa wiki nzima utautumia garage kuliko kazini au kwa familia yako.
Bajeti hiyo unaweza kupaya Harrier old model namba B au C yenye hali nzuri sana..
Nadhani nimeyajenga kwa kiasi changu.[emoji41][emoji41][emoji41]