Kluger na Harrier za mwanzo ni basically gari moja. Tofauti ni mwonekano tu na Harrier ina option ya engine ya 2.1l. So kama unachagua hapo wala usiumize kichwa. Angalia unalopenda mwonekano.
Kwa upande wa Nissans, kama ndio gari lako la kwanza, acha kwanza. Ila kama ni mzoefu unaweza kujaribu. Maana mambo ya kuagiza spare yatakuboa. Na kama mdau mmpja alivyokwambia, Dualis na Qashqai ya chini ya 2014 ni gari moja, majina tu ndio tofauti.
Kwa AWD ya Forester (2008 kuendelea) kwa offroad, hakuna anayetia mguu kati ya hao jamaa wengine. Japo Dualis hayuko mbali saana.