kaka, tatizo lako ni kubwa kuliko nilivyofikiria! kama ni malaria hii ni 10,000 sio 2! hadi chuo hujajua ukikutana kimwili na mwanamke bila kinga atabeba mimba? na sio jukumu lako, ni hesabu 'zao'! Aisee, ngumu kumesa! market ya mwanaume sio kuvaa mashati mazuri na kuwa na bank balance kaka! ni pamoja na uwajibikaji! wa kwanza alikuwa hajui mahesabu, wa pili naye kadhalika! wala hukugundua ungeweza kuenda tuition ukagundua na ww jinsi ya kufanya mahesabu, ukarudia tena! inabidi sasa upate mhandisi kabisa! na mdogo ana miaka 3, unadhani utakayeoa anajua mahesabu manake 3 yrs ago hukujua mahesabu? wasi wasi wangu mkuu ni huu ulowekaji wako na maradhi haya ya sasa. inabidi ujifunze sio mahesabu tu, bali calculus pia! nina wasiwasi hujajifunza kutokana na makosa, na niamini, mwanamke mwenye akili zake timamu atakupiga interviwe hadi ukasirike. nakuandaa tu kukutana na challenges.