Mtoa mada.
Achana na.
1.Jiwe.
2.Nyundo.
3.Spanner (kwanza pikipiki zina toolbox yake ndogo ubavuni)
4.Kisu sijui wamekuambia...
5.Eti mwamvuli
6.Laini kibao za simu,za kazi gani??kuna jamaa wanajua sana kutiana woga asee ni wapi huko unakopita hakuna network??
Haya umeharibikiwa Solya (Manyoni iyo) hizo laini zako zote za simu za kazi gani??utampigia nani??rafiki zako wa Mwanza?wakusaidie nini?
7.Achana na dawa za kuzibia pancha wala kujaza jaza viraka mifukoni,vya nini??unatembea njia gani ambayo haina watu??pancha ya pikipiki inazibwa hata na mafundi baiskeli mzee.
Beba hela tu,ziwe cash kiasi kadhaa na nyingine kwenye mitandao ya simu (inategemea na unaoutumia)
UNAENDESHA PIKIPIKI,NAJUA U AJUA VITU MUHIMU VYA KUVAA KWA AJILI YA USALAMA WAKO SINA HAJA YA KUKUSHAURI,UNAWEZA FUATA USHAURI HAPO JUU.
THEN...
Piga gia mzee unatoboa vizuri kabisa.
Oil ya kubadilisha popote inauzwa mzee,achana na ya kubeba toka mwanza kwanza itapigwa na jua njiani na kulainika kabla ya kuwekwa kwenye injini ndio unakuwa umefanya nini sasa??
KIKUBWA...
Pumzika kila unapohisi,usifanye kama unashindana na kisbo,wao lazma wafike safari yao yaani lazima wafike,wewe hata ukilala njiani haina shida japo unaweza ukatoboa.
KUMBUKA,KILA MAHITAJI UYATAKAYO,YAPO NJIANI.
HAUTOTEMBEA ZAIDI YA KM 50 UKAKOSA MAHITAJI HATA DEMU UNAWEZA KUPATA MBONA WALIOKUSHAURI UJIBEBESHE MAMIZIGO YOOOTE HAYO HAWAJAKUAMBIA BEBA NA DEMU ?(Kuna mtu alishauri japo kiutani)
MANANA YANGU NI KUWA KILA YA AINA YA HITAJI LAKO YAPO KILA SEHEMU.
TEMBEA MZEE BABAH MASUALA YA KUOMBA OMBA USHAURI WAACHIE AKINA @mamadeborah @mamdenyi na wanawake wengine aisee