Nimekuwa katika idara ya elimu kwa miaka kadhaa kama mwalimu,lakini daima siku zote naamini mwenye taaluma zaidi ya moja anajitengenezea vizuri mazingira ya kufanikiwa kimaisha kiurahisi zaidi.
Hivyo nami nawiwa kujiongeza zaidi kwa kusomea masuala ya MUZIKI kama kuimba (kwani nina kipaji hicho na cha kutunga nyimbo), kupiga ala za za muziki/kuwa operator wa vyombo vya muziki.Napenda kusomea masuala ya muziki kwani nina mapenzi nayo na nina imani kuwa muziki ni sanaa ambayo inalipa vizuri kwa sasa.
Je,kwa mawazo haya,unafikiri nimefikiri sahihi/una kipi cha kunishauri?