Forgotten
JF-Expert Member
- Jul 20, 2018
- 3,642
- 11,139
Kama kichwa cha uzi kinavyoeleza... nataka kuunda AI Wrapper itakayoelewa lugha za makabila zaidi ya 125 yanayopatikana Tanzania. Ukweli ni kwamba haitawezekana kwa makabila yote kutokana na aina ya lugha zenyewe, mfano HADZABE.
Kwa wasiofahamu, AI Wrapper kwa lugha nyepesi, ni kuunda mfumo wa teknolojia juu ya Akili Mnemba. Badala ya kuunda Akili Mnemba ya kwako pekee unatumia mifumo ya Akili Mnemba zilizoundwa tayari.
Hili ni wazo la awali linalo-focus zaidi kwenye: cultural-preservation, communication & government services provision. Lengo ni kuwa na versions mbili, free & premium (freemium). Lakini kabla hatujafika kwenye premium lazima kuhakikisha wrapper inatatua changamoto na kuwa na maana kwa watumiaji.
Tatizo kubwa ninaloliona kwasasa Tanzania ni lugha za makabila kupotea taratibu, na sababu kubwa ni muingiliano wa makabila... watoto wengi wanakua kwenye familia baba na mama ni makabila tofauti, kwenye mkoa tofauti na makiba yao, kingine ni lugha hizi kupotea kutokana wazungumzaji kupungua, hivyo inaweza kusaidia kujifunza lugha kwa kutumia Swahili/English translation, pia uwasilishaji wa taarifa na huduma huwa mgumu baadhi ya sehemu Tanzania kutokana na wazawa kutokujua lugha ya Kiswahili, wrapper itakuwa na uwezo wa kuelewa lugha, sauti, na matamshi, hivyo inaweza kusaidia kuuliza taarifa zinazohusu mashirika ya kiserikali, taarifa za ki-afya, ambazo zitakuwa zinakusanywa na kuhaririwa kila pale taarifa mpya zitakapopatikana.
Vitu vya muhimu kuanzia tayari ninavyo:
API
TTS engine
Linguist
Mimi mwenyewe
Time-frame ni miaka miwili, hapo natazamia kuwa na makibila 7 makubwa Tanzania, text-only version inaweza kuwa tayari ndani ya mwaka tu. Kazi kubwa itakuwa kukusanya taarifa za kila lugha nikisaidiwa na Linguist ili kuongeza ufanisi na lugha kuwa fasaha. Baada ya hapo watu wanaozungumza lugha husika watasaidia kuwezesha wrapper kuwa na feature ya Text-to-Speech.
Nime-share hapa ili kupata mawazo ya watu!
Je, ikiundwa AI Wrapper kama hii utatumia?