mmmhh, sijui unapitia nini lakini kwa mie siwezi muanika mme wangu hivi.
Hawara sawa nitamwamnika, mme hell no.
Ni aibu yako, ya watoto, ya ndugu zako, ya ndugu zake, na yeyey mwenyewe.
Kama umeshindwa, kwa nini usifanye maamuzi na kuondoka na kushirikisha familia zenu ukapata haki zako??
Umeamua kumuabisha ili akome? Haikusaidii kwa kweli.
Kwa details ulizotoa hapa sijui magazeti ya udaku yapate, yamwanike ukurasa wa mbele, unadhani watoto wako watasoma huko chuo kwa wiki nzima.
Nimekukasirikia sana wewe mama, ume-act kama mala.ya aliyechukuliwa na mwanamme kwa usiku mmoja, kamwaga mboga umemwaga ugali. Nadhani nafasi ya mke wa ndoa ni zaidi ya hicho ulichofhanya.
Unaamini watu wa hapa kuliko hata nduguzo? Nina maswali kibao, umenishangaza kama mke wa kiaka 21 anaweza fanya hivi.
Kosa la umalaya limefuta wema wake mwingine wote aliowahi kufanyia hadi kumvua nguo hivi? Hebu mkumbuke tangu day 1 anakutongoza, hadi mnaoana, hadi mnapata watoto, hakuna jema hata moja??
Umenikumbusha story ya biblia, abrahamu alivyokuwa anambembeleza malaika wasichome sodoma na gomora. Hata ukikuta watu wema 20, utachoma mji, malaika anajibu hapana, nitawasamehe.
Wewe nawe umekosa hata jema moja la kumsamehe mmeo? Afu usipende kupayuka ukiwa na hasira utajuta siku moja.