Nataka kuvunja ndoa yangu; mme amezidi kwa dogo dogo

Nataka kuvunja ndoa yangu; mme amezidi kwa dogo dogo

Status
Not open for further replies.
Mbona kwa umri wako hufanani na uliyoyaandika? Make haya yanafanywa na watoto wachanga wa ndoa.
 
Mama amechachamaa anataka haki yake...lakini naona kama ingekuwa poa mngeyamaliza wenyewe nyumbani. JF ni uwanja wa fujo...kila kitu kitakuwa wazi soon halafu mhanga atakuwa nani?
 
Mtafute mtu mmoja humu ndani anaitwa Pasco yeye ni mwanasheria wa kujitegemea, anaweza kukupa msaada wa kutosha kisheria.
Pole kwa matatizo.
 
Last edited by a moderator:
mutu mujinga huvunja ndoa yake kwa mikono yake ,maadam umekuja hapa utaokoa ndoa yako ,pengine chanzo ni wewe mwenyewe unamwacha anazuzura muda mwingi bila mpangilio ,jiangalie mwenyewe au umefanya mazoea ,hujirembi tena uko uko tuuuu.matokeo ni hayo amedakwa na wenzio wenye sifa kama zako wao wana nini wewe huna .
 
Talaka ni simu katika maisha hasa katika hatua mliofikia na kupata watoto, hayo matatizo yanazungumzika na kutatulika kuliko kuigawa familia na kupoteza mali zote mlizochuma.
Tafuta watu wa busara na makamu mshauriane pamoja nae kisha kwa wakuu wake wa kazi na hadi katika ngazi za familia yaani ndg walio karibu sana na nyinyi.
Hizo sms si chochote, ni wezi tu hao na usiwape nafasi kwa kuwaachia mume kirahisi hvy just kumbuka enzi zile muwabichi kbs jinsi penzi lenu lilivyokua liking'aa na kupendeza kila kukicha.
Na hata hizo sms za kusema mme wangu zisikupe presha sana ni maneno tu hayo ambayo yanamvuta mumeo hk nje na kingine pia ujichunguze sana hata wewe na utambue ni wapi unakosea au kitu gani umepunguza kumpa hadi kaenda hk kwa hao wngn.
Mwisho ufute wazo la talaka na badala yake utafute dawa ya ndoa yako.
Nendeni kwa viongozi wenu wa dini kwa ushauri wa kiimani zaidi.
 
Kwiwkwikwiwwkwiwkwiwwiwkwiwiwiwwiwwiwkwiwiwiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii
funua funua funua hahahahaahahah funua funua funua
mwagia tindikali huyo mama akae nyumbani asikuchshe bure
 
All in all mama huyu ana haki. Na inaonekana amevumilia sana huyu the so called Jaji!!! I believe jaji huyu ni lazima over 50 years na bado anavulia boxer m.a.l.a.y.a. Liwalo na liwe, Shigongo anika huyu Jaji maana mke ameshasema anataka kuondoka na anatafuta njia ya kisheria ya kufuata. Kwa maisha yalivyo ya hatari siku hizi huwezi kuruhusu uzinzi ndani ya ndoa kiasi hiki. Na hao walioanikwa namba zao hapa ni lazima watakuwa wake za watu au vimada hivyo ni lazima wanaowatafuna wajue. Mpinge nyani bila kumwonea haya.
 
Dadangu pole kwa yote ila ulichokifanya si sahihi kabisa kuweka mambo yenu ya ndani kabisa hapa jamvini, shirikisha watu wachache sana sio kila mtu ataweza kukusaidia, ni-PM tuongee ila naomba futa hii thread italeta madhara makubwa zaidi ya haya.

Mods ili kulinda ndoa na heshima ya Mama huyu naomba hii thread iondoke ili aweze ku-share na watu wachache tu, ni ushauri tu
 
mmmhh, sijui unapitia nini lakini kwa mie siwezi muanika mme wangu hivi.
Hawara sawa nitamwamnika, mme hell no.

Ni aibu yako, ya watoto, ya ndugu zako, ya ndugu zake, na yeyey mwenyewe.

Kama umeshindwa, kwa nini usifanye maamuzi na kuondoka na kushirikisha familia zenu ukapata haki zako??
Umeamua kumuabisha ili akome? Haikusaidii kwa kweli.

Kwa details ulizotoa hapa sijui magazeti ya udaku yapate, yamwanike ukurasa wa mbele, unadhani watoto wako watasoma huko chuo kwa wiki nzima.

Nimekukasirikia sana wewe mama, ume-act kama mala.ya aliyechukuliwa na mwanamme kwa usiku mmoja, kamwaga mboga umemwaga ugali. Nadhani nafasi ya mke wa ndoa ni zaidi ya hicho ulichofhanya.

Unaamini watu wa hapa kuliko hata nduguzo? Nina maswali kibao, umenishangaza kama mke wa kiaka 21 anaweza fanya hivi.

Kosa la umalaya limefuta wema wake mwingine wote aliowahi kufanyia hadi kumvua nguo hivi? Hebu mkumbuke tangu day 1 anakutongoza, hadi mnaoana, hadi mnapata watoto, hakuna jema hata moja??

Umenikumbusha story ya biblia, abrahamu alivyokuwa anambembeleza malaika wasichome sodoma na gomora. Hata ukikuta watu wema 20, utachoma mji, malaika anajibu hapana, nitawasamehe.

Wewe nawe umekosa hata jema moja la kumsamehe mmeo? Afu usipende kupayuka ukiwa na hasira utajuta siku moja.

Umemshambulia mno konnie. . .you just dont know what a desperate mind is capable of doing halafu it seems she is all alone in this hakuna wa kumshauri thats why akaona kimbilio ni jf ndo akatua mzigo wote pwaaa! Mi simlaumu hata kidogo but naomba modes waweke private info nyingne alizotoa. . .I know they know what I mean.
 
Dadangu pole kwa yote ila ulichokifanya si sahihi kabisa kuweka mambo yenu ya ndani kabisa hapa jamvini, shirikisha watu wachache sana sio kila mtu ataweza kukusaidia, ni-PM tuongee ila naomba futa hii thread italeta madhara makubwa zaidi ya haya.

Mods ili kulinda ndoa na heshima ya Mama huyu naomba hii thread iondoke ili aweze ku-share na watu wachache tu, ni ushauri tu
wacha ubinafsi wewe Elli haya ni mambo ya kawaida sana ishewe na nani wengine MBILIA hebu mwaga zile namba nyingine tutakusaidia watoto wamujini ,dontown kitambo tunajua kudeal na wezi sie angekuwaanaheshima angejali na kumheshimu bana
 
Last edited by a moderator:
Basi Mpwa nimefunga bakuli langu mwaya
wacha ubinafsi wewe Elli haya ni mambo ya kawaida sana ishewe na nani wengine MBILIA hebu mwaga zile namba nyingine tutakusaidia watoto wamujini ,dontown kitambo tunajua kudeal na wezi sie angekuwaanaheshima angejali na kumheshimu bana
 
Kuwa kwenye ndoa for 21 years it is not necessarily kwamba mama huyu ni mzee!!suppose aliolewa anamiaka 22 she might only be 43years old!!huyu ni mama tu wa makamo na si mzee!!pole Mbilia kwa hayo yanayokusibu!
 
Nawashukuru sana kwa maoni yenu. ijulikane kuwa ndugu zangu wakubwa wote wamefariki mimi ndo mkubwa sasa. Ktk msg zingine za aliyeolewa zinaonyesha wake na mawifi wakiwasiliana na mwolewaji. Pili nina ngeo ya nyuzi 5 kichwani na ya mdomoni niliona aibu kwenda hospital ili tu nimlindie heshima. Sasa nikiwa mkristo huko kanisani nilikwenda lakini alifika na kuwahonga wachungaji (majina ninayo ili waseme huwa nasali nini huko kanisani), alinambia mwenyewe wakati akiwabeza wachungaji. Nacho hitaji ni ushauri. Huyu ni mtu. Wangapi baba zao walikufa juu ya wasichana ktk magesti house na wapo. Usinibeze hata kidogo, am old enough to ask for your opinions. Ukinibeza nakuona kama ni mmoja wa visichana hivi. we are above 50yrs old.

Ebu kabla ya kunibeza fikiria janga hili la HIV hao watoto wataenda vipi shule? I welcome anyone with positive opinions than humiliations which am suffering from. Usiniongezee hilo.

Thanx. Ni kwa nini mtu aifiche dhambi? Ni maandiko gani yanayotetea dhambi kwa kuificha?
 
Huu hauwezi ukawa ushahidi tosha kuvunja ndoa yako!
Umeshafikiri kuhusu haki zako na mali mlizo chuma pamoja?
Na kushauri utumie njia ya mazungumzo kwanza kabla ya kuruka kwenye kuvunja ndoa!

Pia una takiwa kufikiri kuhusu castody and mantainance of children.( kuhusu matunzo ya watoto kama unao wanao hitaji malezi.
Kama unataka kuvunja ndoa yako
Pia tafuta ushahidi wa kutosha kushawishi mahakama kuvunja ndoa. Mfano hizo sms na ushahidi wa picha utasaidia pia.
Linda sana afya yako!
 
pole mwaya.mpaka umefikia stage hii,nina amini umevumilia vya kutosha.katika maoni sio kila mtu atakuwa upande wako.mume anaepiga hiyo ni dharau tosha.ukiwa kilema,nani atakaekuangalia?mimi sikulaumu.
 
Umeona Smile...wacha atiririke ndio mahawara watajua kama mume wa mtu ni sumu....

mmmh ndo maana sitembeagi na waume za watu mie
wapi global publisher?
eheheeee hao mahawara watakomaje?
acha iwe mbaya mama sema sema!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom