mama unataka msaada wa nini sasa? TUKUSAIDIE NAMNA YA KUVUNJA NDOA AU nini?
nakushauri kitu kimoja cha muhimu sana na ambacho wengi wanaweza wasikwambie. naomba vumilia, miaka 21 ulioishi nae si michache, ni mingi sana sana. na hajaanza leo kutoka nje ya ndoa, pengine alitoka hata kabla hamjafikia miaka miwili kwenye ndoa enzi hizo, hadi leo...meshakuwa wazee tayari, na mna watoto wako chuo. jua kuwa lolote utakalolifanya kuvunja ndoa hii na ktk hatua yeyote ile, halitawaathiri ninyi wawili tu, litawaathiri na watoto wenu na litaweka historia mbaya sana kwenye familia yenu miaka yenu yote. nashangaa unaona msg izo tu halafu unataka kuvunja ndoa. kuna wanawake wenzio wengi walishawakuta kitandani kabisa lakini walivumilia kuendelea na ndoa. bora hata mbadilishe vitanda kila mmoja awe na kitanda chake lakini muendelee kuonekena mmeoana. kwa watoto muonekana hamgombani ila nyie tu ndo mnajua kuwa kila mmoja ana lala kitanda chake huko ndani kama ndo unaogopa ngoma.
kuna rafiki yangu mmoja ana miaka 30 sasaivi, amesoma marekani na hapa. ni mmoja wa watoto wa watu wakubwa tu hapa. mama yake na baba yake waliachana kwa talaka. lakini wale watoto hadi leo hawana raha. hawapendi kusikia kitu kinaitwa ndoa, hata mkiwa kwenye maongezi tu wakaona mnaongelea jinsi wazazi wenu wanavyopendana au wanavyofanya mambo pamoja, anaondoka kwasababu ametengenezewa kidonda cha maisha...kwamba wazazi wake walipeana talaka na yeye ni mtoto wa familia ya talaka.
jaji ni mtu mkubwa tu. jua kuwa, talaka utakayoenda kuiomba mahakamani, itatokea kwenye magazeti, mtajiaibisha tz nzima kwasababu jaji lazima atavumishwa tu na vyombo vya habari. watoto wako watanyoshewa vidole kuwa wazazi wanapeana talaka hawapendani, itawaathiri hata masomo yao hata kama ni wakubwa. sisi watoto huwa hatupendi wazazi watengane hata kama tunawashuhudia wanapigana kila siku home hata mbele yetu. kuna raha sana kuishi na baba na mama nyumba moja kama familia, kuliko kuishi mmoja yuko kule mwingine kule na wamepeana talaka.
ninyi mmeshakuwa wazee, zeekeni pamoja tu. unataka uzeeke na nani? nani atakukuna mgongoni mkono usipofika? unafikiri utapata mzee mwenzio sasaivi? pia, jaji ni jaji. mimi ni mwanasheria...kifupi ni kwamba wanasheria wote huwa tunateteana hata kama ukienda mahakamani, ujue yeye ana watu wengi kuliko wewe, sio kwamba namtetea, ila nisemacho ni kwamba, ujue mahakimu wote utakaopeleka kesi ya talaka yeye ni bosi wao, na watakuwa upande wake, sasa sijui wewe utakuwa na nani, kupambana na jaji mahakamani ni sawa na kupambana na mamba kwenye maji.....mamba majini anawezavuta hata gari, ila nchi kavu hawezi...jaji mahakamani ni kigongo kikubwa sana, ila kwenye mambo mengine ndo anaweza kuwa hana lolote....utakachoambulia hapo ni pale tu yeye akiamua kujifanya mjinga siku ipite, ila ukiona ameamua kula na wewe sambamba, anaweza kukusumbua sana na utaishia kujiaibisha tu na kumwaibisha yeye na watoto wako tu. yaani hapo tunachosubiri toka kwenu ni nyie kuanza kuanikana wee mnajianika mbele ya umma wa watz na watz wakiwacheka tu. cha maana, kaa chini tulia, vumilia, tengana naye kitanda, ila usithubutu talaka. kwanza ni kosa kubwa sana, Mungu hapendi kuachana. uzeeke naye, kama umevumilia miaka yote hiyo, unashindwa nini ssasaivi? ILI WEWE, WATOTO WAKO NA MME WAKO MSIJIANIKE KWENYE UMMA WA WATZ, NAOMBA USIOMBE TALAKA...utajiaibisha tu na utakufa mapema kwa kuumia moyo kwasababu watu hata kama hampendani, kuachana huwa kunaleta stress mbaya sana hata ujizuie namna gani utajikuta umepata kama sio pressure, sukari magonjwa kibao.utapoteza marafiki wengi, utavuruga hata ukoo, ugomvi huo utaenea sehemu kubwa sana utajuta.
halafu, ukiachana naye ndo ataoa kabisa uyo kimada. pia, ujue kuwa, inawezekana kawekewa madawa tu ya libwata, hajui alifanyalo, dawa ikiisha, atarudi kwako akipiga maggoti na kukushukuru kwa kumvumilia..kwasababu si wote wanaotoka nje ya ndoa au wanaooa dogodogo wanakuwa na akili zao, wengine wamevutwa na madawa tu. ushauri huu ni dhahabu.