Nataka kuwa Afisa Elimu Sekondari

Malolella

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2012
Posts
366
Reaction score
114
Wadau heshima kwenu. Nimekuwa nikitamani sana kuwa kiongozi kwenye sekta ya elimu ili niboreshe taaluma kwa vipaji na vipawa nilivyojaliwa na mwenyezi Mungu. Kwa muda mchache ambao nimekuwa kazini kama mwl(1yr) nimeleta mabadiliko makubwa kitaaluma na mfumo mzima wa kiuongozi wa shule na matunda zaidi yanazidi kujitokeza hasa kwnye mitihani ya ndani na nje. Je nitatimizaje ndoto yakuwa afisa elimu ili nioneshe zaidi kipaji changu kwa kuongoza wilaya ili ije kuwa mfano?
 
Huko ni kupenda vyeo badala ya kupenda kazi!sasa kama unaona umefanya mabadiliko mengi huon kwamba ww ndo unafaa kutumikia Taifa badala ya kukaa ofisn na kuzunguka na kt mwaka 1 bado hujatumikia taifa ipasavyo mm nngekuwa kiongoz wako ningekutwisha majukum mengne kwa kukupeleka shule ilyopo mtwara wanafunz wanakoferi sana ukatumikie taifa zaid.
 
Mabadiliko gani? Shule gani? Mkuu Mwanamalundi,tafadhali fika hapa uone jinsi Waalimu wanavyopenda pesa kuliko kazi...
 
Last edited by a moderator:
Piga kazi wewe acha kubwabwaja, mwaka mmoja kazini then unataka cheo kama hicho. Ningekuwa mkuu wako wa shule ningekuteua mwalimu wa darasa form II B.
 
Nimewapata wadau, lakini ndani ya mwaka mmoja nimekuwa mfanyakazi bora wa kanda, naamini ipo siku nitakuwa afisa elimu
 
kila jambo lina wakati wake fanya kazi kwa kiwango chako bila kufikiri vyeo viko mbele yako na hakika utafika utakapo, lakini kwa kukufahamisha tu vyeo vya tz vina sababu zake mmojawapo ni kuwa kada wa chama tawala ama upate wa kukushika mkono usipokuwa kwenye makundi hayo uwe kwenye lile kundi maalum wenyewe wanaliita salama kwa taifa au nyoka lakini pia kuna maeneo ukihonga na kujipendekeza kwa wakubwa cheo kitakujia tu!
 
Piga kazi wewe acha kubwabwaja, mwaka mmoja kazini then unataka cheo kama hicho. Ningekuwa mkuu wako wa shule ningekuteua mwalimu wa darasa form II B.

Mkuu alinipa umakamu ndani ya miezi mi4. Nimefanya changes mpaka shule jirani wanakuja kujifunza kwetu....na hvi juzi nimeorganize training kwa walimu inayohusu ufundishaji kwa njia shirikishi kwani njia hizi ziki2mika vizuri humfanya mwanafunzi kuelewa zaidi kuliko ku2mia direct approach. Semina ilihudhuriwa na walimu wote wa wilaya akiwemo afisa elimu sekondari. Mbali na kuniingizia kipato lakini pia nataka wilaya ye2 iwe mfano kitaaluma ndiyo maana napenda zaidi niwe afisa elimu ili nisimamie elimu vizuri na kwa uhuru.
 
sasa wewe mbona una haraka hivyo???
Mafanikio makubwa hayapimwi kwa mwaka mmoja ndugu yangu
Fanya kazi chunga tamaa mbaya
 
hongera mkuu....nina amini kitu kiitwacho fate so mkuu kama imepangwa iwe ivyo; 1 day yes.
 
Elimu yetu haihitaji mabadiliko ya mwaka mmoja inahitaji maono ya muda mrefu,halafu sidhani kama unaweza kuleta mabadiliko katika elimu kwa sababu hata jinsi ya kutimiza ndoto zako tu hujui utawezaje kuleta mabadiliko ya wengine kama yako tu unashindwa.Halafu hayo mafanikio ya mwaka mmoja sidhani kama ni yako nahisi ni ya wenzako uliowakuta.Watoto wengi wanafeli kwa sababu waliokosa base nzuri ya form one mpaka form three,we unasema umetoa matunda in one year!!!!! hiyo ni questionable?
 
Kama ni kweli hapo ulipo naona unatumika vizuri komaa hapo hapo nadhani ndo utawasidia vizuri,kama nia yakokweli ni kuwasaidia watz
 
Mmetoa one ngapi mkuu na mekuwa wa Ngapi kitaifa kuna A ngapi za Sayansi na Hisabati?
 

Nimekupata.SI NDO WEWE ULIOTUSEMINISHA UKATUPATIA MI VYETI YAKO AMBAYO HUKUISAINI! NA PESA TULIKULIPA!
 
Una ugonjwa unaitwa Adminsyndrome, ni ugonjwa wa kupenda uongozi kuliko kufanya kazi.

Dogo una mwaka mmoja tu wa kazi umeshaanza kuwazia Uongozi wa juu namna hiyo! Bila shaka utakuwa msumbufu hata kwa Mwalimu wako Mkuu.

Wenzako wana DECADES ndani ya fani hawana ndoto hizo, cheo hicho hukitafuti kinakuja chenyewe kwa kuteuliwa tu, chapakazi watu waione dogo.
 
Weka takwimu sio kuloloma, weka jina la shule na ni binafsi au ya serikali? na hayo mafanikio ni ya mwaka gani? Je ulileta wewe peke yako au na walimu wenzio? Weka hapa tukupigie promo kama unastahili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…