Nataka kuwa machinga wa kike ushauri

Tembeza vivalio
Au accecories

Tembeza michezo ya watoto

Tembeza visandles vya kike

Tembeza nguo za ndani za wanaume kwa wanawake na watoto

Tembeza samaki waliokaangwa

Tembeza nguo za watoto za mtumba

Vingine nimesahau.
Sio kwa mtaji wa elfu 20 mkuu. Angalau angekuwa na 200k
 
Kama una ujasiri pia amka asubuhi nenda ilala
Chukua nyanya,vitunguu
Dagaa,
Nyanya chungu
Bamia
Karoti
Limao/ndimu

Pita mitaani mpaka saa sita umefunga hesabu
Angalau wewe nimekuelewa vyema. Anza na hii mishe vinginevyo wewe ndo utakuwa bidhaa.
 
Habarini wajasiliamali

Mimi ni mwanamke wa miaka 29 nataka nianze biashara ya umachinga naombeni ushauri biashara gani inatoka sana huko mitaani hasa maeneo ya mjini kama kariakoo kwa mtaji wa elf 20

Mimi niko mkoani Arusha
Elfu 20[emoji54]
 
Hizo chupa tu za kuuzia uji zinazidi elfu 20. Bado vikombe na unga wa uji na viungo vyake.
Chupa hata za nyumban anaazia na vikombe
Hapo mchele nusu na robo. 2000
Unga wa ulezi au walishe (Ikibidi atengeneze Mwenyewe) kilo Mbili Hauzidi 10000 mazagazaga yote mpaka kusaga
Sukari kilo 2200
Maziwa Lita huko moshi yamejaa Kibao
Imebaki 5400 ataangalia hii anunue vikombe vya 500 , vya kuazia Inayobak anaweka.

Tatizo Mkuu umekalii 20000 Pesa nyingi kwa hizi biashara ndogo ndogo
 
Uchumi wa raia wa hiyo mitaa ukoje? chunguza kitu gani kina miss hapo ukifanyie kazi utapata wateja wengi. Pia tafiti wanapenda kula, kunywa au kuvaa au kutumia vitu gani na ni adimu hayo maeneo?

Ukifahamu hizo gaps nakuhakikishia dada biashara yako itakwenda vizuri kwani uhakika wa kuuza vitu unao.
Faida nyingine utajibrand vizuri na utafahamika coz utakua unique kwenye biashara ya hivo vitu.

Muhimu: Angalia usalama wa hiyo mitaa usijeibiwa mtaji wako na usalama wa maisha yako in advance, vibaka ni wengi sana unajua maisha ni magumu so nyie wanawake majambazi wanafahamu ni rahisi kuwapokonya bidhaa.

Good luck...
 
Subiri nikuongezee nyingine

Uza maandazi au vitumbua asubuhi unayachoma kumi na Mbili asubuhi uko barabarani unatembeza.

Biashara ya mahindi ya kuchemsha unachemsha weka Kwenye ndoo mida ya jion ingia barabaran.

Ungekuwa Dar Hiyo 20000
Unaenda karume au Ilala unapoint nguo za 1000 mpk 3000 . Ukiingia mtaani unaziuza 5000 kwenda juu
 
Nimekusoma mkuu. Shikamoo 20000. Naona watanzania sasa tuna nidhamu na pesa.
Mkuu usiachie spana endelea kukaza vyuma vilivyolegea.
 
Nimekusoma mkuu. Shikamoo 20000. Naona watanzania sasa tuna nidhamu na pesa.
Mkuu usiachie spana endelea kukaza vyuma vilivyolegea.

Hahaaaaaaa wanyonge hizi Ndio biashara zetu tangu Enzi za mzee kipara huko tushazoea kusulubika waliozoea mteremko 20000 kwake ni Pesa ya soda Sasa Ndio wanahaha
 
Hahaaaaaaa wanyonge hizi Ndio biashara zetu tangu Enzi za mzee kipara huko tushazoea kusulubika waliozoea mteremko 20000 kwake ni Pesa ya soda Sasa Ndio wanahaha
Ila una aidia sana kwenye swala la biashara. Nimekupenda bure mkuu.
Sijui nipeleke posa maana ukiwa na mke wa type yako lazima utoboe tu maisha hata kama huna mtaji wa kueleweka.
 
Habarini wajasiliamali

Mimi ni mwanamke wa miaka 29 nataka nianze biashara ya umachinga naombeni ushauri biashara gani inatoka sana huko mitaani hasa maeneo ya mjini kama kariakoo kwa mtaji wa elf 20

Mimi niko mkoani Arusha
Rais mmoja wa nchi za africa mashariki aliwahi kuwambia wanawake "utajiri mnao mmeukalia," uliielewa kauli hiyo?
 
Nilipita pale mji mdogo wa karatu nikaona mdada mmoja mzuri mrembo kweli kweli ni machinga anauza vitu vyake
 
Tembeza vivalio
Au accecories

Tembeza michezo ya watoto

Tembeza visandles vya kike

Tembeza nguo za ndani za wanaume kwa wanawake na watoto

Tembeza samaki waliokaangwa

Tembeza nguo za watoto za mtumba

Vingine nimesahau.
Hauna akili unajua e? Hivi fedha halali kwa malipo ya shilingi elfu 20 inaweza fanya yote hayo au umejiskia kupayuka?.
 
Hauna akili unajua e? Hivi fedha halali kwa malipo ya shilingi elfu 20 inaweza fanya yote hayo au umejiskia kupayuka?.
Hongera mwenye akili
Millionea wa jf.
 
Fnya food processing! Nunua viungo mbalimbali vya kupikia kma nyanya, vitunguu, karot, hoho n so on then vioshe na kuvipaki vizuri alafu pita kwenye maofisi mbalimbali! /
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…