Nataka kwenda Dubai au China kununua simu nipeni maelekezo mliowahi kwenda

Unaweza kununua hiace kwa hiyo pesa, ukiendesha mwenyewe uwezo wa kulaza 80-100 kwa siku unao kwa 100%.
 
Nauli toka Dar hadi Guangzhou ni kuanzia dollar 1200 hapo inategemea na siku hiyo ni go return

Nashauri pakia Ethiopia maana inatoa Kg nyingi.

Hii waweza book na kulipia mwenyewe au utembelee ofisi za Ethiopia. Mawakala huwa wanaongeza dollar 100 kwa kila ticket.

Ukifika Guangzhou uamuzi ni wako
Ukipakia Taxi utalipa hela nyingi inaweza fika 100 hadi 300yuan kama Laki hivi ili ufike Kati kati.

Au utumie Train yenyewe ni bei rahisi nadhani ni yuani chini ya 50


Hotel pia uchaguzi ni wako zipo ambazo utakuwa watu weusi ndio wengi na hizo bei zake ni ndogo kwa siku na zipo hotel za bei kubwa kazi kwako.

Kuhusu chakula kuna kihotel kwa Mtz wanapika chakula cha Ktz hapo Guangzhou.

Kutembezwa sokoni kuna Watz wako huko ila ndo hivyo ukienda nao wanakuongezea bei.

Kutuma mzigo unaweza kuja nao ila TRA airport hawatakuacha salama.
Au
Unalipia kwa Kg hao watz wanakutolea kwa dollar 10 kwa kila mzigo au 20000 kwa kila simu.
Wao wanajua wanavyofanya huko airport.
 
Kwangu hii ndiyo ushauri mzuri
 
Watanzania wengi ni watu wawivu mno

1. Nauli kwenda na kurudi: USD 1,200

2. Chakula kwa siku: USD 22

3. Hotel Single Room: USD 50

4. Nauli ya mizunguko town: USD 49
(Taxi+Metro+Daladala)

5. Mzigo wako unaotaka kununua: (Na
hii tukupe jibu?): Minimum USD3,500
 
SALALY ndiyo nini mkuu? rudi shule hata ya watu wazima unatuaibisha mabaharia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…