Heshima yenu brothers and sisters. Baada ya kumaliza chuo na kusota mtaani kidogo niliajiriwa na private company kuanzia 2013 hadi 2018 kampuni ilipofirisika na kufunga shughuli zake nchini (kipindi cha mwendazake).
Nikajikita kwenye biashara ya mavazi ya kike na kiume na vitu mf. handbags, viatu nk, japo mtaani pesa ilikuwa ngumu sana kipindi hicho lakini si haba biashara ilinipa matumaini. Mapema tu nikaanza kusafiri kuchukua mzigo China&South Africa, tena kuna wakati nikahisi nilichelewa kuanza hii biashara. Changamoto ya Corona ikaingia na hapo mambo yakaanza kuwa magumu (upatikanaji wa mzigo ikawa shida na nikiagiza inachukua hadi miezi 3 kupata mzigo, mauzo yakapungua pia).
Ikafika wakati matumizi binafsi yakaielemea biashara ikawa haikui na mzunguko ukawa slow sana yaani mtaji nazungusha uleule ila faida yote inaishia kwenye matumizi kifamilia na jamii hivyo, nikaamua nitafute ajira walau nipunguze mzigo kwa biashara.
Mungu ni mwema, 2020 nikapata ajira kwenye private company nyingine japo ujira wake ulikuwa mdogo ila nikajipa moyo nipambane hivyohivyo huenda baraka zingine nitakutana nazo huko kwenye ajira mpya. Nimefanya hii kazi kwa miaka2 sasa lakini sioni nikiendelea kiuchumi wala kiujuzi, faida pekee naipata ni bima ya afya kwa mama yangu. Natumia muda mwingi sana kazini kiasi nashindwa kusimamia biashara yangu vizuri (niliajiri mtu dukani), ni kazi yenye day na night shifts hii pia inanipa wakati mgumu sana maana nina familia. Imefikia wakati naona sina future na hii kazi na katika kufikiria nina wazo hili japo kuna wakati nahisi ni uamuzi wa busara ila kuna hofu fulani inanijia kwamba nisije kujutia baadae.. naomba ushauri wenu[emoji116]
Nataka niache kazi, nitafute goli kariakoo niendeleze biashara hii hii ya nguo za kike. Kwa sasa nchi nyingi mipaka imefunguka hii inanipa matumaini nikipambana mwenyewe kwa uzoefu mdogo nilionao nitapata zaidi ukilinganisha na ajira ninayofanya hivi sasa. Hofu ninayoipata nikiacha ajira bima ya afya ya mama itasitishwa ilihali afya yake ni dhaifu na huugua mara kwa mara[emoji848] na sijui katika mapambano yangu nitafanikisha lini kumkatia bima binafsi maana ugonjwa hauna hodi....... nisaidieni mawazo wanafamilia
Shukrani