Nataka niache kazi ya ualimu, naombeni ushauri.

Kwa sasa nakushauri uendelee na kazi yako ya ualimu huku ukianzisha biashara ambayo itakuwa karibu nawe ili iwe rahisi kwa wewe kuifuatilia. Baada ya kuona biashara yako imesimama vyema na inalipa vizuri zaidi kuliko ualimu, hapo ndio wakati sahihi wakufanya maamuzi.
Note:
Hakikisha umeisoma biashara yako kwa kipindi angalau cha mwaka mmoja na usifanye biashara ambayo hauna idea nayo kabisa
 
Kama unapata 430,000 kwa mwezi ACHA KAZI Mkuu, Ukiacha utaanza kupata 999999999999999999999999999999999999999999999999999999999000000000000000000000000000000000000000000000000000000000000000000000000000000
hahahaha we hiyo namba inasomwaje?
 
asante sana mkuu
 
Usiombe ushauri wa kuacha kazi. Tafuta mtaji ukiupata uje uombe ushauri wa kuanzisha mradi au biashara. Kazi utaacha tu mwenyewe pale mafanikio ukiyapata
 
Ckushauri uache kazi mkuu ila buni biashara ambayo utaicmamia mwenyew hakikisha unachokipata hapo hupeleki ktk matumizi yoyote unaendlea kuizungusha ikipatikana faida kubwa unasogea ktk mradi mkubwa kuliko huo, lkn pia kama unafanyia kazi mikoani unaweza kununua mazao baada ya mavuno ukayaweka kwa muda wa miez 5...ukapata faida nzuri sana, ukiwa kazini unaweza kukopa ukaendlea kupiga kazi ukatoka jiwekee malengo tu. Kuna walimu kama ww waliweka malengo Leo mill 30 haziwapigi chenga na hawana mpango wakuacha kazi, kaza buti
 
Usiuradhau huo mshahara unaoupata ukiacha kazi na ulishazoea lk4 znaingia baada ya wiki NNE tunaokufaham tunaweza kuhic unaumwa
 
Unakofundisha wanaokuzunguka vijana wenzao wana maendeleo Kama wanalima nawe lima
 
Aaisee kaka ukweli hamna kabisa maana matumizi yamekuwa makali sana ukizingatia familia zetu za kusaidiana yaani umekuwa mtihani mkubwa, ila tokea nianze kuwanza hili nimeanza kuweka akiba mwaka huu january mpaka nimefikisha laki 9 tu
Fanya mambo mengi kwa wakati mmoja.huku ukiwa na uhakika wa kwenda ATM.kila mwezi.tafuta washauri wa mambo ya ujasiriamali.uanzishe biashara.huku ukiendelea na kazi.usiache kazi.bora nusu mkate.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…