Nataka nianze biashara ya kuuza ugali na dagaa mchele

Nataka nianze biashara ya kuuza ugali na dagaa mchele

aise

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2018
Posts
5,175
Reaction score
16,488
Wakuu,

Nataka nianze kuuza ugali na dagaa mchele wale wa kukaanga, nitaweka na kachumbari kunogesha au mboga za majani.

Nimefikiria ugali na nyama ya kukaanga lakini nimeona itanikost sana kwenye nyama. Kwahiyo mbadala nimeona ni dagaa mchele ambao kuwapata ni hapa hapa Kigamboni. Kuna mwenye uzoefu na hii biashara?

Nimefikiria nikauzie sehemu wanayouza chakula bei juu, mimi nipeleke pale kwa Buku ni ugali, dagaa mchele na kachumbari.
 
Anza haraka sana mambo mengine yatakaa sawa mbele ya safari huko kwa kuongezea wachanganye kwa kuwapa rosti la nyanya chungu na bamia na maji ya kandoro bure.Simu moja tu mkuu tukutane benki.
 
Kuna mwenye uzoefu na hii biashara?

Nimefikiria nikauzi

Kwahiyo nini kama Mwanza wameanza siku nyingi? Asifanye hiyo biashara au? Mchawi wewe
Anaongea kitu ambacho kipo tayari kama ni kitu kipya !! Ameuliza uzoefu ndio nikampa mfano wa mkoa wa Mwanza ugali dagaa Mchele uko kila kona mijini na vijijini na bei yake ni elfu moja kwa sahani.
 
Anaongea kitu ambacho kipo tayari kama ni kitu kipya !! Ameuliza uzoefu ndio nikampa mfano wa mkoa wa Mwanza ugali dagaa Mchele uko kila kona mijini na vijijini na bei yake ni elfu moja.
Kwenda zako. Umemwambia "wewe ndio inaota leo?". Halafu umeshaona anauliza kwa wazoefu wamwelekeze maana yake anajua sio kitu kipya ndio maana ameulizia wenye uzoefu.

Acha uchawi.
 
Good idea ndugu yangu hata haapa k.koo msimbaz kuna wamama wanauza ugali buku buku wana wateja wengi sana
 
Mimi huwa nikikaa na mtu anaependa kujaribu kufanya biashara huwa namwambia usiulize sana utakata tamaa au utakatishwa tamaa so natoaga ushauri wa we anza tu biashara kila mtu na bahati yake.
 
Back
Top Bottom