Nataka nianze biashara ya kuuza ugali na dagaa mchele

Nataka nianze biashara ya kuuza ugali na dagaa mchele

Wakuu,

Nataka nianze kuuza ugali na dagaa mchele wale wa kukaanga, nitaweka na kachumbari kunogesha au mboga za majani.

Nimefikiria ugali na nyama ya kukaanga lakini nimeona itanikost sana kwenye nyama.

Kwahiyo mbadala nimeona ni dagaa mchele ambao kuwapata ni hapa hapa Kigamboni.

Kuna mwenye uzoefu na hii biashara?

Nimefikiria nikauzie sehemu wanayouza chakula bei juu, mimi nipeleke pale kwa Buku ni ugali, dagaa mchele na kachumbari.
Kwa buku na bei ya unga sasa itakukata walau buku jex
 
Bonge la idea kuna wadau wako pale karibu na Meeda Sinza wanauza sana ugali, dagaa mchele na kachumbari mida ya usiku. Cha muhimu upate location yenye mzunguko wa watu
 
Back
Top Bottom