Nataka nianze ujasiriamli nikiwa chuo

Hehe heee

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2017
Posts
213
Reaction score
186
Habari zenu wana jamvi mimi ni mwanachuo wa mwaka wapili apa UDOM kwasasa nina 200,000/= ambayo nataitafutia kibiashara au shughuri yoyote ya ku invest hii pesa ili inizararishie na huu ndio utakuwa mwanzo wangu wa kufanya kwa vitendo na kuwacha day dream tu

Nawasilisha

NB: Biashara hiyo sio lazima iwe ndani ya chuo ata nje ya chuo
 
Kabla ya kuangalia biashara itakayokupa faida kwa haraka naomba nikushauri kidogo

Ili ufanikiwe kwenye biashara lazima uwe na nidhamu na matumizi yako

Nakushauri iyo laki mbili nunua vocha yakurusha kwanza hapo haina faida sana lakini ni njia moja wapo ya kujifunza jinsi ya kuzuia matumizi yako

Ukiweza kukaa na biashara iyo zaidi ya miezi mitatu bila kudhuru mtaji basi utakua umekomaa

Kwanza kwa hapo chuoni utakua umeshajijengea jina,uta Julikana na watu wengi kwaiyo hata ukija kuanzisha biashara nyingine

Mimi huwa naamini na nitaendelea kuamini kua mtaji
wa biashara yoyote ile ni wateja na sio bidhaa,
 


Asante mkuu kwa mawazo yako mazuri
 
Safi sana dogo,

Una laptop? kama unayo unaweza kufanya yafuatayo;

1. Nunua printer, kisha unaweka chumbani kwako. Wanafunzi wenzako wote ambao mpo block moja uwafahamishe kuwa una print, mlango wa chumba chako weka tangazo kuwa una print pamoja na namba yako ya simu. Wale wanafunzi wote wazima moto watakuwa wanakuja kwako kuprint usiku na weekend ukiwepo. Hulipii umeme wala frem, printer za laki mbili zipo kibao tu.
2. Hiyo ya kwanza ikienda vizuri save pesa, nunua printer ya kuprint picha (vile vidogo havizidi laki mbili) kisha nunua camera yako unaanza kupiga wanafunzi wenzio passport size za dakika tatu. First year wakifungua chuo unaweza kuongea na bank iliyokaribu nawewe unakaa nje ya bank kwaajili ya kupiga passport size wanafunzi
3. Hiyo moja na mbili zikifanikiwa uwe unakusanya pesa, baada ya muda fulani weka tigo pesa na mpesa chumbani kwako. Wakija kuprint wanatoa na pesa.

Sikuwa na akili hiyo chuo, ningekuwa nayo ningekuwa sijawahi kutembeza CV, usifanye makosa tuliyoyafanya kaka zako. Kila la kheri dogo
 
Kwa vile unamawazo kama yangu naomba nami nikuoe wazo ambalo mimi nimefanya.
mimi ni mwaka wa kwanza na nilichokifanya baada tu ya kuchuku boom ya kwanza nikatuma 600000 sehem kwa ajiri ya kuwekeza kwenye kilimo cha mpunga uko morogoro ambapo nitalima hekari 2 kwa hela izo ni kuanzia kukod shamba mbegu,dawa,na kulima, nikirud kwako inakubd uangalie wewe kama wew ufanyaje kulingana na mazingira unayotoka,pamoja na mahitaji ya wanaokuzunguka.
Mwisho hongera kwa kuamua kuandaa mazingira ya kujiajiri .
 
Uzi huu unanifanya niwe na amani sana
 
Safi sana nami umeniongezea changamoto katika maisha barikiwa sana mkuu
 
wakati wa kulima uende, wakati wa kupanda uende na uwe na tabia ya kwenda shamba mara kwa mara. kilimo cha remote control kutegemea kutuma pesa na kula faida utakuja kulia kilio cha kusaga na mawe, utaona ni bora ungenunua iPhone. Kilimo kinahitaji usimamizi na sio kutuma pesa tu, sikukatishi tamaa bali nakuelezea uhalisia
 
Biashara zinachanganya sana ubongo mdogo wangu. Kufanya ujasiriamali ukiwa chuo ni kujitafutia kudisco tu!
si kweli, acha kumfundisha uoga. Asifanye biashara za kusafiri akawa anakosa masomo na test, anaweza asiwe A student akawa C student lakini sio kudisco maana ili udisco chuo kunahitaji juhudi kubwa na maarifa.
 
Kama ni mdada naona kuna opportunity kwa sasa ukiwa chuo unaweza kufanya japo inahitaji kidogo upate mafunzo, kwa upande wa kina dada zetu kwa sasa make up imeshika kasi sana kama unavyojua chuoni sherehe hazikosekani kama picnic, wengine wanatoka out hasa siku za weekend unaweza kuwa unawafanyia make up kabla hawajaenda kwenye mitoko yao na ukatengeneza pesa kwa muda huo wa ziada! but inatakiwa upate mafunzo namna ya kuwaremba kulingana na ngozi zao then ukishaelewa unanunua vitendea kazi! yangu ni hayo kwa sasa!
 


Asante bro nitalikalia chini wazo lako kulifanyia kazi
 


Yaap kilimo ndio target yangu kuu na ndomana nataka nikusanye mtaji niingie kwenye iyo field ya kilimo
 
Kama ni mtoto wa kike tafadhali fata ushauri huu, start up capital ni ndogo sana na return yake ni kubwa. Safi sana mdau
 
Ila hapo ken makosa hapana.... Hamna kosa mlofanya hata hela ya boom kama ndo targeted capital sio nyingi aisee sema kama unataka kufanikiwa lzm ujibane Sana
 
umeniwah,,,kilimo na ufugaji sio kutuma tuma pesa tu, yalinikuta mwaka jana,mwaka huu sifanyi makosa.
 
mkuu,angaliiaaa, pesa Mwanaharamuu sanaa
 
kuongezea tu, ukishakua bize na shuuli zako hua kuna kusahau kipi hasa kimekuleta pale, uta disco, au kupata masup mengi, jarib ku balance mda wako vizuri katika shule/biashara
ni hayo tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…