Safi sana dogo,
Una laptop? kama unayo unaweza kufanya yafuatayo;
1. Nunua printer, kisha unaweka chumbani kwako. Wanafunzi wenzako wote ambao mpo block moja uwafahamishe kuwa una print, mlango wa chumba chako weka tangazo kuwa una print pamoja na namba yako ya simu. Wale wanafunzi wote wazima moto watakuwa wanakuja kwako kuprint usiku na weekend ukiwepo. Hulipii umeme wala frem, printer za laki mbili zipo kibao tu.
2. Hiyo ya kwanza ikienda vizuri save pesa, nunua printer ya kuprint picha (vile vidogo havizidi laki mbili) kisha nunua camera yako unaanza kupiga wanafunzi wenzio passport size za dakika tatu. First year wakifungua chuo unaweza kuongea na bank iliyokaribu nawewe unakaa nje ya bank kwaajili ya kupiga passport size wanafunzi
3. Hiyo moja na mbili zikifanikiwa uwe unakusanya pesa, baada ya muda fulani weka tigo pesa na mpesa chumbani kwako. Wakija kuprint wanatoa na pesa.
Sikuwa na akili hiyo chuo, ningekuwa nayo ningekuwa sijawahi kutembeza CV, usifanye makosa tuliyoyafanya kaka zako. Kila la kheri dogo