kingphisher
Member
- Nov 30, 2024
- 45
- 79
Wakuu habarini za wakati huu. Husika na madam tajwa hapo juu, Nina elimu ya Shahada ya kwanza katika tasnia ya teknolojia ya habari na biashara. (Businesses Information Technology).
Usiku wa kuamkia Leo nimekosa usingizi baada ya kuwa na mawazo ya kuwaza na kuwazua juu ya maisha yangu ya usoni. Nimeamka nikaenda magotini nikasali na kukaa. Ilikuwa ni saa name usiku, baada ya hapo nikawa nawaza cha kufanya. Baadaye nikapata wazo.
WAZO LANGU: Niende Benki kuu (BOT) niombe Mkopo angalau milioni mia 4-5 ninunue mabasi mawili ya mikoani, au
Niende benki ya taifa ya biashara. (NBC) niwaelezee dhamira yangu ya kuomba Mkopo wanipe mlioni 10 - 20 nianzishe biashara ya nguo.
Hayo mawazo mawili yamenisumbua Sana usiku mzima na sijalala wakuu. Japo kwa upande mwingine naona kama ni jambo gumu. Kabla sijaachana nalo, nimeona nije humu nione mnipe miongozo iliyotukuka na ushauri mwanana juu ya hata mawazo yangu mawili.
.Natamani kujua: Je, kwa mtu ambaye siye mtumishi Wa serikali anaweza kuomba Mkopo BOT na kupewa?
.Je, kwa mtu ambaye si mfanya biashara, ambaye Ana ndoto kama zangul anaweza kuomba na kupewa Mkopo kutoka hizi benki nyingine (NBC, NMB, CRDB ......?)
Naombeni ushauri wakuu. Natamani nijiajiri ila mtaji unanitoa jasho.