Nataka nifanye maamuzi magumu ya kutengana na mke wangu

Nataka nifanye maamuzi magumu ya kutengana na mke wangu

Naona umesemea ya kwake

Angekuwepo tumsome na yeye!
 
Tuishi nao kwa akili. Hivyo tu.

Mwanamke (sio wote) kwa asilimia kubwa huangalia SASA....hawana kumbukumbu ya wakati uliopita. Na siku zote wako sahihi, hawajawahi kosea!!

Mwache aburudike, iko siku atajua kuwa aliruka mkojo na kudandia kinyesi.
 
Hilo zimwi umelifuga. Shemeji yako alipoanza dharau ilitakiwa umtimue haraka sana. Halafu mke wake naye angeleta maneno, ungemwambia naye aungane na mdogo.

Listen brother. Wanawake mara nyingine wanatabia kama za watoto, kukujaribu kuona boundaries zako. Usipokaza sura na moyo utachezewa. Mke wako mpaka anatoa mimba! Wewe upo tu.
 
Inaelekea wewe ni mpole sana,mkeo na ndugu zake washaujua huu udhaifu wako,wana take advantage of, huyo mwanamke ni selfish (anataka uhudumie Kwao tu) katili mpaka kuua Kiumbe kisicho na hatia sababu ya pesa??.. na kama ameweza hili anashindwaje kukucheat??? My brother sipendagi kuona mahusiano yanavunjika ila hapa inabidi tu uondoke Tena kwa speed kubwa ,huyo MWANAMKE HAKUPENDI,anakutumia tu,siku UKIPOTEZA KAZI au KUCHACHA jua atakufukuza ndani ya nyumba kama mwizi,sauti ya wengi sauti ya Mungu..achana nae
 
Ukichunguza wengi mnaoleta visa vya wake zenu humu ni kwamba mmeowa "watumishi".

Kuna Mzee Mmoja hata hanijui aliwahi kuniambia "tafuta asiyesoma sana utadumu naye". Hawa wasomi sio wanawake wazuri kwa ndoa.

Namrudia Aisha wangu class 7 mwenye kipaji cha hali ya juu.
 
Mkuu mimi siwezi kushauri muachane kwa kuwa sijui vema dhamira yenu ya kuoana.. ila nadhani mnachopishana hapo ni kiburi... mwanamke kiburi na mwanaume kiburi... angalien namna ya kumaliza tofaut zenu, msiishi kama maadui, haipendez, kila mmoja atambue wajibu wake na kuutimiza kwa kadri ya uwezo wake. Lakini pia, kila moja ajue msingi wa ndoa na kuzingatia...

Usione wazee wetu wanaishi kwenye ndoa kwa miaka 40, ukadhani hawana matatizo.. suluhsho la tatizo syo kulikimbia

Acha kumdanganya mwenzio,au mpaka aletewe ukimwi ndani sababu ya pesa ndio urealize kuwa amefanya makosa kuwa na huyo mwanamke? Hello
 
Ukichunguza wengi mnaoleta visa vya wake zenu humu ni kwamba mmeowa "watumishi".

Kuna Mzee Mmoja hata hanijui aliwahi kuniambia "tafuta asiyesoma sana utadumu naye". Hawa wasomi sio wanawake wazuri kwa ndoa.

Namrudia Aisha wangu class 7 mwenye kipaji cha hali ya juu.

Ngoja ukute class 7 ,afu ana kiburi ndio utashika adabu,lol
 
Members naomba tu niandike kwa ufupi naamini mtanielewa na kama kuna ushauri nakaribisha.

Tumebahatika kupata mtoto mmoja 5yrs now, wote ni watumishi.

2013 akaomba nimsaidie kumtafutia shule mdogo wake wa kiume arudie kidato cha pili baada ya kufeli form four na kukaa nyumbani miaka karibu mitatu nikafanya hivyo, baada ya muda shemeji akaanza dharau na kiburi kwangu tena mbele ya Dada yake, nikilalamika Dada mtu anachukulia poa, nikavumilia baada ya muda mfupi kapigwa suspension akapiga magoti nimsaidie asifukuzwe shule, nilipoona habadiliki nikajitoa kumsaidia but ilikuwa ni baada ya Dada yake kusema kama naona taabu ye atalipa ninamsema sana mdogo wake.

Dogo kamaliza na division 3 point 26, wakaomba chuo cha afya government wakakosa, huruma ikanijia nikamwambia Dada mtu aende private kidato cha tano akakataa akakomalia kuwa anampeleka chuo cha afya private kama 4 million ada na mahitaji mengine nikamwambia haitawezekana hali ni ngumu kiuchumi aende advance.... nikaambulia matusi kuwa nina "gubu" na maendeleo ya mdogo wake na nisijali yeye na ndugu zake watalipa ( by this time tulikuwa tupo mbali sababu za uhamisho), mi nikaona nisiingilie ndugu.

Kumbe hakuna lolote yeye ndo mlipaji wa kila kitu, nikaja jua baadaye kuwa amekopa bank bila kunijulisha na pesa sijajua kafanyia nini kumuuliza anasema anasomesha......sijakaa sawa kumbe alikokuwa mwanzo kakopa pesa za watu million mbili kwa ajili ya jambo hilo na hajarejesha hadi sasa pamoja na riba inafika nearly 4 million.

Ametoa mimba ili aweze kujikeep busy na biashara nje ya kazi ili kuweza kugharamia masomo ya mdogo wake nilipobaini anasema maisha magumu tusubiri kwanza nilipombana anasema bahati mbaya....uwongo...

Nilisafiri nikarudi ghafla bila taarifa nakuta anaongea na mwanaume kwa simu SAA saba usiku tena anamwomba amsaidie pesa alipe ada......

Mbaya zaidi nyumbani kwangu amegoma kusaidia chochote anasema si kazi yake kufanya majukumu ya kifamilia Mimi kama baba natakiwa nitekeleze kila kitu akifanya ni huruma tu.....

Kila linaloendelea kwangu anawajulisha ndugu zake ( baba, mama na Dada zake), nikichukua hatua hata za kumzaba kidogo ili tuheshimiane basi kesho asubuhi kama ilikuwa ni usiku ntapokea simu za hao watu wakinishutumu nikiwaeleza yaliyojili inaonekana mi ndo nakosea....

Amesafir kikazi wiki ya tatu sasa simu hapokei, SMS, hajibu akipokea haongei....

Namsubir arudi niite ndugu pande zote mbili niwambie nimeshindwa....kweli wanaume tumeumbwa mateso!!


It always boils down to economics!

Ndoa ikishakua na mchanganyiko na ndugu lazima ikufe!

Im really sorry this is happening!
 
Back
Top Bottom