Nataka nifanye maamuzi magumu ya kutengana na mke wangu

Nataka nifanye maamuzi magumu ya kutengana na mke wangu

Usikimbilie kufikiria kumuacha.

Hapo ni kuwaita wakubwa/ watu ambao wanaweza kuwa na heshima kwenu na wote mkaweza kusikiliza wanachowaambia. Wanaweza kuwa wazazi, mshenga, viongozi wa kanisa nk.

Kila mmoja aeleze kwa undani jambo linalompa changamoto katika ndoa yenu.

Mtafika mwisho mzuri naamini. Kuachana ni hatua ya mbali sana kama mliamua kuoana kwa ridhaa yenu wenyewe na sio kwa kulazimishwa.

Mungu ni Mwema.

Mungu anatenda

Msiache pia kumshirikisha
Uwa anajibu kwa wakati hawai wala hachelewi.
Huu ushauri sio mzuri kabis
 
Asante....ni nyumba ya kupanga, kiuhalisia financially simtegemei cause ameweka nguvu kwao kusomesha na kuwajengea wazazi wake, kwa sasa tupo pamoja baada ya kufanikiwa uhamisho mwaka jana

Okay, pole sana.

Hayo maisha yatakuwa magumu kwa sababu hawezi kubadilika, na wazazi/ndugu zake wanakuona kama adui kwa sababu unaonekana kukwamisha msaada kwao.

Tafuta hela, kapange kwingine, mwachie kila unachoona kinafaa kubaki, kama akisema na mtoto umchukue fanya arrangement, akikubali kubaki naye endelea kuhudumia mpaka utakapoona una mazingira mazuri ya kukaa naye.
 
Kila linaloendelea kwangu anawajulisha ndugu zake ( baba, mama na Dada zake), nikichukua hatua hata za kumzaba kidogo ili tuheshimiane basi kesho asubuhi kama ilikuwa ni usiku ntapokea simu za hao watu wakinishutumu nikiwaeleza yaliyojili inaonekana mi ndo nakosea....

Amesafir kikazi wiki ya tatu sasa simu hapokei, SMS, hajibu akipokea haongei....

Namsubir arudi niite ndugu pande zote mbili niwambie nimeshindwa....kweli wanaume tumeumbwa mateso!!


Hapo unafuga Simba ndani ya nyumba!
Sidhani kuna haja ya kuitisha ndugu kwako kwanza. Weka mipaka vizuri na usijejikuta umechelewa ingawa yaonekana umeshachelewa. Ila kumwacha muda bado!
 
Mkuu mimi siwezi kushauri muachane kwa kuwa sijui vema dhamira yenu ya kuoana.. ila nadhani mnachopishana hapo ni kiburi... mwanamke kiburi na mwanaume kiburi... angalien namna ya kumaliza tofaut zenu, msiishi kama maadui, haipendez, kila mmoja atambue wajibu wake na kuutimiza kwa kadri ya uwezo wake. Lakini pia, kila moja ajue msingi wa ndoa na kuzingatia...

Usione wazee wetu wanaishi kwenye ndoa kwa miaka 40, ukadhani hawana matatizo.. suluhsho la tatizo syo kulikimbia
Hapa hakimbii tatizo mkuu,bali ana solve tatizo.Kumuacha ni moja kati ya njia nzuri za kusolve tatizo.Tena njia bora mno.
 
Na nyie mnaheshimu wake zenu au mnataka Kuwa Mungu mtu. Wanaume wa siku hizi hamujielewi kabisa ujue. Kila siku kulia lia mkiona mke kawazidi hata elimu mnaanza kuji feel inferior na kulaumu. Unataka good package wakati package yako mbovu tu
Yaani hivyo vitu viwili ulivyoorodhesha ndiyo kila kitu Mkuu. Bahati mbaya akina dada zetu wa sasa wanachukulia poa sana (hasa suala la heshima kwa mume). Mume haitaji vitu vingi kutoka kwa mkewe, anachohitaji ni ile "imani" kuwa mkewe anamuheshimu na kuiheshimu kauli inayotoka kinywani mwake. Ninachoamini wanamume wanaoheshimiwa na wake zao na kutokea kutengana huwa "wanajuta sana"
 
Mmh km kaweka nguvu kwao hamna kitu hapo! Unapoteza muda,yupo ki maslahi
Asante....ni nyumba ya kupanga, kiuhalisia financially simtegemei cause ameweka nguvu kwao kusomesha na kuwajengea wazazi wake, kwa sasa tupo pamoja baada ya kufanikiwa uhamisho mwaka jana
 
Umenena vyema yani kwa yote hayo bado unaomba ushauri? ni bora umegundua mapema fukuza huyo anza maisha mapya ndugu
Haya ndiyo madhara ya wanaume kupiga magoti wakati wa kuwavisha pete wake zao. Unapandwa kichwani since day one.

Wewe hapo hukuoa uliolewa, fukuza haraka sana uende kanisani ukajichagulie mtoto mbichi mkali sana atakayesuuza moyo wako.
 
Mke anachukua mkopo kwa siri, hataki msaidiane maswala ya famili, hakuna future hapo ndugu, piga chini akaishi na ndugu zake huko.
 
Mke anachukua mkopo kwa siri, hataki msaidiane maswala ya famili, hakuna future hapo ndugu, piga chini akaishi na ndugu zake huko.
 
Wanaume mnapenda sana mwanamke asiyejitambua
Ili umfanye kama rimoti unabonyeza tu

You don't accept challenges from us

Yaani mwanamke kukopa bank bila kumpa taarifa mumewe ndo kujitambua?

Mwanamke kutoa ujauzito akiwa ndani ya ndo ndo kujitambua???

Mwanamke kutokupokea simu kwa muda wote huo tena kwa mumeo ndo kujitambua?

Hivi ninyi mnaichukuliaje kujitambua

Ndo maana wahuni hatuoi tunatupia tu kama kawaida mkisema sisi waoga yeah sisi waoga wa kuwa na wanawake wanaojitambua kwa ujinga
 
Members naomba tu niandike kwa ufupi naamini mtanielewa na kama kuna ushauri nakaribisha.

Tumebahatika kupata mtoto mmoja 5yrs now, wote ni watumishi.

2013 akaomba nimsaidie kumtafutia shule mdogo wake wa kiume arudie kidato cha pili baada ya kufeli form four na kukaa nyumbani miaka karibu mitatu nikafanya hivyo, baada ya muda shemeji akaanza dharau na kiburi kwangu tena mbele ya Dada yake, nikilalamika Dada mtu anachukulia poa, nikavumilia baada ya muda mfupi kapigwa suspension akapiga magoti nimsaidie asifukuzwe shule, nilipoona habadiliki nikajitoa kumsaidia but ilikuwa ni baada ya Dada yake kusema kama naona taabu ye atalipa ninamsema sana mdogo wake.

Dogo kamaliza na division 3 point 26, wakaomba chuo cha afya government wakakosa, huruma ikanijia nikamwambia Dada mtu aende private kidato cha tano akakataa akakomalia kuwa anampeleka chuo cha afya private kama 4 million ada na mahitaji mengine nikamwambia haitawezekana hali ni ngumu kiuchumi aende advance.... nikaambulia matusi kuwa nina "gubu" na maendeleo ya mdogo wake na nisijali yeye na ndugu zake watalipa ( by this time tulikuwa tupo mbali sababu za uhamisho), mi nikaona nisiingilie ndugu.

Kumbe hakuna lolote yeye ndo mlipaji wa kila kitu, nikaja jua baadaye kuwa amekopa bank bila kunijulisha na pesa sijajua kafanyia nini kumuuliza anasema anasomesha......sijakaa sawa kumbe alikokuwa mwanzo kakopa pesa za watu million mbili kwa ajili ya jambo hilo na hajarejesha hadi sasa pamoja na riba inafika nearly 4 million.

Ametoa mimba ili aweze kujikeep busy na biashara nje ya kazi ili kuweza kugharamia masomo ya mdogo wake nilipobaini anasema maisha magumu tusubiri kwanza nilipombana anasema bahati mbaya....uwongo...

Nilisafiri nikarudi ghafla bila taarifa nakuta anaongea na mwanaume kwa simu SAA saba usiku tena anamwomba amsaidie pesa alipe ada......

Mbaya zaidi nyumbani kwangu amegoma kusaidia chochote anasema si kazi yake kufanya majukumu ya kifamilia Mimi kama baba natakiwa nitekeleze kila kitu akifanya ni huruma tu.....

Kila linaloendelea kwangu anawajulisha ndugu zake ( baba, mama na Dada zake), nikichukua hatua hata za kumzaba kidogo ili tuheshimiane basi kesho asubuhi kama ilikuwa ni usiku ntapokea simu za hao watu wakinishutumu nikiwaeleza yaliyojili inaonekana mi ndo nakosea....

Amesafir kikazi wiki ya tatu sasa simu hapokei, SMS, hajibu akipokea haongei....

Namsubir arudi niite ndugu pande zote mbili niwambie nimeshindwa....kweli wanaume tumeumbwa mateso!!
Umekuwa mvumilivu Sana bro ndoa kitu gani .unataka uishi maisha mafupi kwaajili ya mwanamke halafu katoa mimba yako yaani kaua mwanao ili asomeshe mdogo wake. Ukiendelea kuvumilia hesabia siku zako za kuishi ni chache Duniani. Mtoto wa kiume haitakiwi uhangaike hivyo. Ukiachana nae kwani utakufa au utashindwa kuishi . Itisha kikao cha familia mwambie it's over . Tena usimsamehe kabisa. Atakufanya uwe maskini
 
Yaani mwanamke kukopa bank bila kumpa taarifa mumewe ndo kujitambua?

Mwanamke kutoa ujauzito akiwa ndani ya ndo ndo kujitambua???

Mwanamke kutokupokea simu kwa muda wote huo tena kwa mumeo ndo kujitambua?

Hivi ninyi mnaichukuliaje kujitambua

Ndo maana wahuni hatuoi tunatupia tu kama kawaida mkisema sisi waoga yeah sisi waoga wa kuwa na wanawake wanaojitambua kwa ujinga
Huyo mwanamke ANAFUNGISHA boss!!!!!
 
Ukioa mwanamke anatakiwa kujihusisha na mambo ya kwao kwa ruhusa yako.
Ukiona anafanya kwa kuamua na ndugu zake Basi Ni afadhali akaishi na ndugu zake tu ijulikane moja.

Labda uniambie alijilipia mahari
 
Back
Top Bottom